AH! Mbona huelewi wewe? Elimu yako iko juu ya Uingereza na Marekani tu hivyo hata pasipo na mfanano basi utataja huko. Hebu tupe mlingano kati ya Uingereza na Marekani na ule wa Tanzania.
Kwa taarifa yako muungano wa Tanganyika na Zanzibar unashadidiana sana na wa Uingereza.
Uingereza or United Kingdom inajumuisha England, Scotland, Wales, Nothern Ireland, Isle of man. Sisi hapa Tanzania muungano wetu ni Tanganyika na Zanzibar. Kwa miaka 47 yote ya muungano state visits zimekuwa zinafanywa na Tanzania, sio Tanganyika au Zanzibar na kuna vitu kibao tume copy kwa waingereza. Huyu Bimani hajazaliwa leo, na wala hajaanza siasa leo, sasa iwaje analalamika kwa huu ujio wa Prime minister wa India? Kwa nini asilalamike alipokuja rais wa Somalia? au hata alipokuja George Bush?
Pia nijuavyo mimi India wana ubalozi mdogo Zanzibar, kwa nini hajapeleka malalamiko yake huko? Naibu waziri wa mambo ya nchi za nje 'Mahadhi' ni mzanzibari, huyu Bimani anaweza kulalamika. Hata hivyo nahisi Bimani anawalilisha kundi fulani na hii hoja yake ni mwendelezo wa chokochoko za muda mrefu.