CUF inazidi kujidhihirisha ni CCM-B | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF inazidi kujidhihirisha ni CCM-B

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Aug 27, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Inanitatiza hapa. Inakuaje - katika vyama vikuu vya upinzani – CUF inaonekana kulala usingizi?

  Hivi hili pingamizi Dr Slaa alilomuwekea JK kuhusu "hongo" kwa wafanyakazi CUF wao hawakuliona? Au ndiyo wanafanya kampeni zao za ki-uswahiba na CCM kufuatia "ndoa" yao (ya CCM na CUF) ya kule jikoni?

  CUF wasijidanganye – CCM haina uswahiba kabisa na mtu hasa inapohusu kuachia madaraka.

  Kule Visiwani, CUF wanakwepa kuweka pingamizi kuhusu ugombea wa Dr Shein pamoja na kwamba hana sifa za ugombea kule (chini ya Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar) kutokana na ukweli kwamba hakujiandikisha kama mpiga kura kule.

  CUF watakuja juta. CCM na ZEC yake inaweza ikacheza rafu mbaya katika mchakato wa uteuzi wa wagombea katika uchaguzi huko, na CUF, kutokana na "ndoa" hiyo, wakashindwa kuweka pingamizi hivyo wagombea wa CCM wote wakapita bila kupingwa. Kwa nini CUF wanajibweteka kiasi hiki? CCM ina chembe gani ya uadilifu kukumbatiwa kiasi hicho?


  Tuliona jinsi CUF, huku bara mwaka 2000 jinsi ilivyokuwa tishio kwa CCM hadi chama hicho tawala kikawa kinatumia mabavu kukikandamiza na kukisingizia kutega mabomu katika maeneo kadha jijini Dar. Lakini sasa hivi CCM haioni kama CUF ni tishio kwake na wao (CUF) wanalijua hilo.

   
 2. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Nia ya watanzania wengi ni mabadiliko katika uongozi wanchi yetu. Na kwa sasa mabadiliko hayo yanawezekana kupitia vyama vya siasa tu. Hivyo sio vyema kila kukicha wafuasi wa vyama vya upinzani kusemana semana; tuwekeze nguvu zetu katika kuelimisha umma wa watanzania. Kwa kuzingatia ufinyu wa rasli mali na uhuru wa kutekeleza kazi za siasa hapa nchini kazi ya kuelimisha umma haiwezi kufanywa na chama kimoja ni lazima kushirikiana. Chama hiki kikiwa huku kingine kiwe kule.

  Kwa mtazamo huo hoja yako haina matiki yoyote waache waendelee na kusukuma gurudumu la mabadiliko
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Yeah -- mabadiliko yatapatikana -- huku baadhi ya vyama vinanunuliwa na chama tawala!!!!
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wewe zungumzia chadema yako. mbona huko nyuma mlikuwa hamzungumzii CUF. CUF walipigwa kila walipokwenda na kunadiwa kuwa ni chama cha kidini na hata mwenyekiti wao Prof. Lipumba alivunjwa hata mkono (malipo ya serikali ya Mkapa) hamkuongea leo hii unakuja na CUF ni CCM B? What? kwani wewe kinakuuma nini hata kama ni CCM C, do your busness mdada achana na CUF, yenyewe ina viongozi makini, wafuasi imara (si wanafiki) ambao hawageukagi nyuma siku zote. Huwezi linganisha na chadema yako inayoibuka kama uyoga na naamini itapotea hivyo hivyo kama ilivyoibuka. We shall see, and the time will tell.
   
 5. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #5
  Aug 28, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndugu Ngwendu,

  Nadhani hujui historia ya Chadema vizuri, CHADEMA NI CHAMA ambacho kimekuwepo mda mrefu na wamekuwa wakijitahidi kuimarisha chama kwa mda mrefu na hata kwenye chaguzi mbili za 1995, and 2000 hawakuweka mgombea Uraisi na waliunga mkono Wagombea wa NCCR-MAGEUZI na CUF, hivyo hicho ni chama makini ambacho kilikuwa na malengo ya mda mrefu sio kukurupuka tu, hivyo basi CHADEMA ilipofika hapa leo ni kutokana na strategies na kazi kubwa iliyofanyika na viongozi wengi wa chadema, angalia hata transfer of power ya viongozi wa chadema ni ya kizalendo na makini, viongozi wamekuwa wakibadilika toka mwenyekiti MTEI, then BOB NYANGE MAKANI na leo ni Mbowe, Lakini CUF tunaona ma sultani miaka nenda rudi, tafikiri CUF ni mali ya SHARIF HAMAD na LIPUMBA hakuna mwislamu mwingine safi anaeweza kuwa kiongozi wa CUF miako yote?

  Chadema haina deni kwa CUF bali CUF ina deni kwa Chadema, kwani chadema imekwisha toa support kwa CUF na Lipumba amekataliwa na wananchi SINCE 1995, 2000, AND 2005 so hana jipya ni kuwapotezea wananchi kura zao kwani kushinda kwa Pro Lipumba is a very long shot na they know it, ni kitu ambacho hakiwezi kutokea basi tu kwasababu CUF wamenunuliwa na CCM na kupewa danganya toto ya serikali ya mseto ambapo SHEIKH SHARIF atakuwa makamo wa RAISI ambaye hana kazi na ni powerless, sasa kwa sababu wanachama wa CUF ni mbumbumbu hawajui kuwa huo ni ulaji na utukufu wa viongozi wao na kuwarahisishia CCM kuendelea kutawala milele kwa kuwaweka kwapani viongozi wa CUF,
   
 6. S

  Selemani JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2010
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Upinzani makini ni changamoto kwa maendeleo ya nchi. Lakini hapa kwetu hatuna upinzani makini. Mnagombana wenyewe kwa wenyewe and expect mtanzania makini awape kura yake.
   
 7. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu unaongelea Bob Makani yupi? Yule akina mrema walisema kuwa CUF na chadema ni vyama cha kidini hata Makani anaitwa Bob Mohamed Makani? Huo ndo muungano unaoongelea? Siona kama kuna deni hapa kwa kashfa mlizowavalisha wana-CUF. Labda tu ni rudie kusema yale yaliyowakuta CUF ndo yatakayowakuta chadema. Tena afadhali hata ya CUF mengi yalikuwa yakusingiziwa lakini kwa chadema mambo yapo waziwazi na ukweli wake upo clear, wala hakuna kificho. we'll see.
   
 8. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CUF Imekosa viongozi walio makini kufuatilia jambo..hasa wanasheria waliobobea...!
   
 9. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2010
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwani hilo pingamizi limeshawekwa? Mbona hatuna taarifa zozote za pingamizi hilo hata Jana kwenye kampeni M Marando alisema atawasilisha Pingamizi hilo Jumatatu.

  Sasa tueleze mwanzilishi wa mada hii pingamizi gani hilo lililowasilishwa?
   
 10. Zungu la Unga

  Zungu la Unga Member

  #10
  Aug 29, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muflis hawa wote wanaoishutumu CUF. Siku zote hizo walikuwa CCM mpaka juzi juzi tu walipogundua kuwa washapigwa chini ndani ya CCM na waakina Yusufu na Halfani. Ndiyo maana wengine wanashindwa kuzuia hisia zako na unawasikia wakidai hao "Waswahili" waondolewe Ikulu. Akiondoka Mswahili mmoja, Mkwere, anaingia Mswahili mwengine, Mnyamwezi.

  Pingamizi ni kutaka ushindi wa mezani... Nyinyi si mnadai "mmebadilisha upepo wa kisiasa"? Sasa mbona mnakimbilia kwa kamisaa kutaka pointi tatu bila ya hata mechi kuchezwa?

  Eti CUF hawana wanasheria? Kama wanasheria wenyewe ndiyo hao wanaotetea mafisadi mahakamani basi ni bora tusiwe na hao wanasheria uchwara.

  [my first post hapa JF]
   
Loading...