CUF ina mkosi gani?

CUF ina mkosi gani?

CuF chama letu kubwa, si unaona tumeshalamba urais huku Zanzibar? Tuhangaikie tena nini? Sasa hivi tuna kazi moja kubwa tuliyopewa na Rais JK, nayo ni kusambaratisha upinzani kwa namna yeyote ili kuwahakikishia mabwana zetu CCM utawala wa milele.
 
Jamani bado nauliza CUF ina matatizo gani?
 
UDINI! UDINI! UDINI! UDINI!! Mkuu udini utakuteketeza! Kama huwezi kusakata kabumbu kaa juu ya jukwaa upige makofi na kuwashangilia wanaume zako.

kwaio CUF wameshindwa kusakata kabumbu,ivo wameamua kukaa jukwaani kuwashangilia mabwana zao Sisiem?
 
Jamani bado nauliza CUF ina matatizo gani?
Kwani nini chanzo cha swali lako mkuu

Haina matatizo ila viongozi wake ndiyo wenye matatizo.....Na sasa wanampango wa kukiua kabisaaa ktk ramani ya vyama vya siasa nchini au ktk orodha ya vyama vya upinzani ,,,,matokeo utokeo utayapata muda si mrefu subiri
 
Strategies zao zilikua ni madaraka zaidi na njaa kali na ugumu wa maisha maradhi umri na kuzeeka vibaya ambalo ni tatizo kubwa sana kwa sisi waafrica,once the edge rise up the capacity of thinking rise down,tofauti na wenzetu wazungu unakuta kadiri umri unavyozidi kukua na ubongo nao unachapa kazi kwa speed ya hali ya juu.yuko wapi maalim seif,wapi shamsi vuai,enzizile ulikua ukitamka cuf unasikia na harufu ya damu,nilikua mdogo na mfano tuliokua tunatishwa nao ni mauaji ya rwanda hivyo tukawa hatutaki kusikia cuf wala maalim seif kwani tulijua wanataka kutuua kama wanyarwanda.maalim alienda kutibiwa ulaya na sisemu aliporudi nafikiri hata kadi ya sisiemu alipwa kimtindo.kilichobaki nikuelekeza nguvu zote chadema kwani plani yao imejipanga vizuri sana alafu watu wana muono wakitaifa zaidi na sio wa kiitikadi au jamii ya watu flani au kundi flani kama ilivyokua kwa cuf.
 
Kama itafikia hatua ya kusambaratika..kama ilivyokuwa NCCR,basi wale wapinzani wa kweli wapokelewe CDM! Mfano J. Mtatiro,na hata Prof Lipumba! Yule mchumi ni wa muhimu sana..
 
CUF iko 'Apolo India' kwa muda mrefu sasa, tuwe na subra wakati tunasubiri taarifa za madaktari.
 
hapa ni uroho wa madaraka tu hamna kingine. Nashut down
 
Siisikii CUF zanzibar na mikashikashi yake huku bara ndiyo kabisaa sijawahi waona huku mikoani tangu uchaguzi mkuu uishe zaidi ya uchaguzi wa Igunga walipopata aibu ya karne. Iko wapi ile CUF ya Mapalala iliyotingisha serikali bara na visiwani hadi kulazimika serikali kuingiza watu wao kuisambalatisha, ile CUF ya Seif imeenda wapi, labda sasa tutegemee hii mpya inayokuja ya Hamad Rashid. Hakika tunahitaji chama kingine cha tatu chenye nguvu baada ya CCM na Chadema.
Acha visambaratike vibaki vikubwa viwili ili tupate nguvu kubwa ya kuiangusha CCM, by the way CUF sio chama cha kukitegemea tena ktk vyama vya upinzani. Kimeshapoteza mvuto kwa jamii, hasa Tanzania Bara, sijui visiwani labda bado wanakielewa.
 
Ha ha ha ha ha! Mbona bado kidogo sana; wako chini ya uangalizi maalumu wa daktari - complete bed rest. Mkuu bado kitambo kidogo sana utasikia vigelegele kama mtoto atafanana na baba au matusi na talaka kama atakuwa na nywele za singa.

Ultra sound imeonesha wana mimba ya pacha - CUF-HR (CCM-D) na CUF-SH (CCM-B original) ila mmoja kakaa vibaya, katanguliza masaburi. Kaa mkao wa kula.

ahaaa kumbe wanahitaji upasuaji basi ili kuokoa maisha ya mama na watoto pacha, nahisi dr. CHADEMA atafaa sana kufanya upasuaji huo katika hospitali kuu ya TUNDU LISSU katika mkoa wa ZITTO wilaya ya Mnyika
 
Back
Top Bottom