CUF imeshindwa kwa sababu hizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF imeshindwa kwa sababu hizi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jamesbond007, Sep 17, 2012.

 1. jamesbond007

  jamesbond007 Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1. Athari za uandikishaji 2010.

  Hakuna mabadiliko yoyote ni orodha ile ile ambayo wanachama wengi wa CUF hasa majimbo yenye nguvu hawakuandikishwa licha ya kelele zote zilizipigwa. Ukweli ni kwamba hiyo idadi ya matarajio ya Tume na watu walioandikishwa 9000 bububu. zaidi ya nusu si wakaazi wake, hapajafanyika uchambuzi wa wa kina tokea uchaguzi wa 2010 mbinu ni zile zile tu. Vitambulisho ni sahihi lakini watu wamepandikizwa na ccm hili wanalijuwa.

  MBINU YAO. mamluki hutoka majimbo yao yenye nguvu kunakuwa na rest ya watu kwa makundikuanzia 50 hawaandikishwi katika majimbo yao ahlisi lakini huingizwa katika list kufididia majimbo mengine. mkakati huu umekuwa ukifanywa kwa ustadi mkubwa baina ya waandamizi wa chama na watu wa idara nyeti ikishirikiana na baadhi ya maofisa wa tume (sio wote) hasa waliomo ktk idara ya takwimu.. Ustadi ni mkubwa kwa sababu huepuka makosa yote . Mkakati ni kutowaandikisha wakaazi halisi wote kwa visingizio tele kutoka kwa masheha na ilikuficha kuonekana jimboni kuwa watu wengi hawajaandikishwa hio idadi huwekwa kwa kulinganisha watu wa eneo na hujazwa kwa kuingizwa hao mamluki. ubaya wa mambo vyama kikiwemo CUf wameshindwa kujuwa typical sura kwa sura wasio wakaazi kwa sababu picha za wenye vitambulisho ni sahihi na vitambulisho ni sahihi lakini wakaazi ni mapandikizi.

  CUF lifanyieni kazi iwe ndio kazi yenu kuu kipindi hiki mtakubaliana nami huko baadae. taarifa hizi nimezipata kwa rafiki yangu ambae ni mwandamizi (idara ya mipango na Takwimu) si rahisi kujuwa watu wanacheza na data .Hebu niulize swali. Hivi CUF licha ya kuwa na mabuku ya watu walioandikishwa wamewahi kufanya survey kwa njia zao ili kubaini hili? ni ngumu lakini inawezekana wao hufanya makisio ya kujuwa wanachama wao walioandikishwa halafu hujipa matumaini ya uishindi kwa kuangalia kuungwa kwao mkono na umati . wengi wa hao hawajaandikishwa. ndivyo ilivyo bububu. CCM wameandikisha wanachama wao wopte hata watoto wadogo na ili kupata kura za ushindi wana make balance kwa kuongeza mamluki ambao bila kufanya survey ya kufa mtu kaya kwa kaya si rahis ikugunduwa siku ya kura sura ndizo na vitambulisho ni halali siku hizi hawapori visanduku na wala hawabahatishi.

  2. Kutumiwa vikosi kukamilisha mkakati wa ushindi. hili kila mmoja analijuwa fuatilieni mujuwe ukweli.

  Mimi nilidhani baada ya GNU hili lisingekuwepo (CUF hawajawa na Athari katika serikali) Askari wamedhihirisha chukiyao na ukerekwetwa wao. Angalia jana Pale betrasi geti la karibu na mshelishelini mpaka waziri wa cuf na naibu waziri fulani( Majina tunayo0 wanafoka kuhusu hujuma bado askari hata habari hawana. wananchi wakiwa wamedhibitiwa na askari wako mbali wanapiga kelele huyo siye huyo siye wanawajuwa lakini kmkm wanawapitisha kwa kuangalia vitambulisho tu ndio nikasema kuna mapandikizi yaliyohalalishwa na CUF hawajuwi. Mageti yote mawili walikjuwa askari kmkm peke yao FFU wao wakizunguka na magari tu.

  USHAHIDI WA HILI
  Nimeshudia magari 2 kwa nyakati tofauti moja canter limebeba watu linaingiya likiongozwa na jgari la jeshi ambapo waliokuwemo hawakupekuliwa hata kutazamwa vitambulisho vyao wananchi kule wanapiga kelele hao sio.- Pale mlangoni alikuwepo askari mmoja hakuvaa uniform nilidhani ni wakala wa chama fulani lakini nilifuatilia baadae nikajuwa ni askari kwa sbabu walikuwepo wasio na fomu jana . yule jamaa alikuwa muda wote anahaha baina ya askari wenzake wenye fomuna huu upande wa raia akifanya mawasiliano na baadhi ya watu. Mara moja mh Muwakilishi wa micheweni anakaguwa gari yeye huku anawaruhusu watu kupita bila kufanyiwa ukaguzi wa kina si mara moja wala mbili. jamaa huyu nilimfuatilia sana mnamo saa 11 na dakika 25 pale maskani ya ccm iliyopo karibu na ikulu ya kibweni nilimkuta anapongezwa na kupewa pole kwa kazi aliyofanya” ahsante sana na pole kwa kazi nzito ………tizama wambie watoke hao wawili uwapeleke wanakwenda kiembe samaki gari ile pale” ilisika kauli moja kwa mshajihishaji pale maskani sikuweza kumtambuwa mara moja.

  - Pale kibweni kmkm ilikuwa kama pana karamu vespa na baiskeli nyingi watu wengi walivaa kiraia hasa wanawake na kila wakati gari likitoka na baadhi yao kuelekea vituoni. hawa bila wasiwasi wakipiga kura kama sehemu ya mkakati kwamba ni watu wa bububu na wanavitambulisho halali.Cuf HILI HAWAKULIONA ILIKUWA VIJANA WAMEHEMKWA TU PALE VITUONI HUKU NJE YA UWANJA HAWAONI. kwa kweli hiyo ndio hali.

  Mkakati wa Ulinzi kufeli.
  Walijiyahidi vijana wa CUF kudhibiti hali pale asubuhi na kulikuwa na ishara ya fujo lakini baadae polisi wakadhibiti na ndio kukawa mwanya baadae wakachukuwa nafasi kmkm na ndio ukawa mwiba zaidi, Nilimuona muwakilishi anahaha pekee akikaguwa gari huku watu wanapita na kmkm wanaruhusu mh hakuwa na wenziwe pale wanachama walifukuzwa. hawa waheshimiwa wengine walikuwa wapi.? kituo hiki ndio kimetowa ushindi wa CCM ingawa wengine wengi waliogopa vishindo vya mitama na magumi pale asubuhi kutoka kwa vijana ambao baadae walitawanywa.
  - nk

  NINI KIFANYIKE?
  1. CUF haraka itumie ushawishi wake katk GNU (kama wanao0)suala la uandikishaji liwe safi hata kuundiwa tume maalumu ya baraza la wawakilishi litayumbisha GNU huko mbele.

  2.Licha ya kukataa matokeo waweke pingamizimahakamani na wafanye Survey niliyosema watayajuwa majina na sura za mamluki ingawa muda hautotosha Result ndio uwe ushahidi wa kukataa matokeo na sababu nyengine nyingi za ufujaji zilizojitokeza.( Kazi hii ilitakiwa ifanywe baada tu ya Uchaguzi mkuu au kabla ili sample zipatikane kwa uhalisia ) jimbo la bububu kwa sasa liwe mfano.
  Waimarishe chama ngazi za chini wengi wa wafuasi wao ni wa mkumbo na waimarishe kitengo cha takwimu kwa kuwatumia vijana na idara ya takwimu huo uwe ndio mpango mzima wa sasa. sio kila siku mikutano ya hadhara tu fanyeni maandalizi ya kutwaa nchi sasa hili la DATA ni muhimu ,UANDIKISHAJI pamoja na USIMAMIAJI KURA maandalizi yafanywe sasa nje ya serikali (chama ) na ndani ya GNU huu ni mtihani kwa GNU yenyewe.

  Nawasilisha
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kinachoi'cost CUF ni ndoa yake na CCM.
  Kabla ya kufanya lolote kwanza ivunje hiyo ndoa yake ya mkeka.
   
 3. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ndio maana sikipendi chama cha mabwepande (CCM). majizi makubwa haya.
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kama vile unapenda waZenji waendelee kuuana! doubt.
   
 5. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  halafu mkuu umekosea jukwaa la kuleta habari yako pamoja na maudhui na uzuri iliyonayo. hapa habari inayouza ni ya chadema tu. waG ni watu waajabu sana kuliko unavyofikiria. kuna mmoja aliandika na naona ameondoa huo mchango katika huu uzi "mambo ya ngoswe" na kwa lugha ya haraka haraka ni kwamba huu uzi si stahili hapa.
   
 6. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Hii thread najua itahamia kwenye udini tu. Subirini muone
   
 7. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  waG ni Wagalatia....
   
 8. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,193
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  si cuf wanavuna walichopanda jamani! Umelewa mtaa wa wabakaji, kweli utachwa kubakwa?
   
 9. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,193
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni kweli! Rainaa Hawa hata mbaazi ukikosa maua husingizia CDM!
   
 10. N

  Nabihu JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Wahifidhina wanataka kuirudisha znz ilipotoka ni hatar sn hawa.
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  CUF ni mfu hata Zanzibar hakikubaliki! RIP uamsho
   
 12. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,193
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  ahahahahaa! nakupa5 Mkuu!
   
 13. k

  kamili JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 714
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Kabla ya uchaguzi wa mwaka 2000, nilikuwa naishi Muheza na kuna watu waliandikishwa kwenye daftari la wapiga kura la Zanzibar, Shuhuli hio ilikuwa inafanyika usiku kwenye ofisi za CCM vijijini. Kilichonishangaza japo kuwa mgombea wa CUF wa kipindi hicho ( kwa sasa amehamia CCM) alifahamishwa kuhusu suala hilo, si chama cha CUF au yeye binafsi alilishulikia.
   
 14. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #14
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  kwani kuuana kumeisha?
   
 15. k

  kamili JF-Expert Member

  #15
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 714
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Mkuu CHADEMA bila ya vyama vingine tutakuwa tunakirudisha CCM madarakani kwa jina lingine. Na pia umakini wa CHADEMA utakuwa na kasoro kama hawakujifunza kutoka streghth and weakness za CUF katika chaguzi zilizopita.

  Kila chama kinachodhamiria kunyakua madaraka kutoka CCM ni muhimu wajifunze hila walizotumia CCM dhidi ya CUF.A au chama kingine kitaangukia kwenye hila zile zile zilizowadondosha CUF. Mjinga hujifunza kupitia makosa yake mwenyewe wakati mjanja hujifinza kupitia makosa ya wengine.
   
 16. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #16
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  we muongea pumba kumbe upo? siku hizi upo kimya sana(japo wewe na mimi ni kama mafuta na maji).
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Walahi ni kama Mbingu na Akhera.
   
 18. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,844
  Trophy Points: 280
  Duh!demokrasia ya hii nchi kweli hatari.
   
Loading...