BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,331
Hakuna chama chochote cha siasa kikubwa ambacho hakina migogoro ya ndani. Hata CCM wana migogoro ya ndani na ushahidi ni kufukuzwa kwa hivi karibuni kwa baadhi ya Wakongwe ndani ya chama hicho akiwemo Mwenyekiti wa UWT ambaye pia amepoteza Ubunge wake na kauli za hivi karibuni kama hizi za Kinana na Bashe.
Huyu Lipumba alishajiuzulu ndani ya chama na akawaita waandishi wa habari kujiuzulu kwake na pia kupeleka barua CUF kuhusu kujiuzulu kwake. Baada ya kujiuzulu akataka kurudi ndani ya chama kinyemela na akakataliwa na CUF wakatumia taratibu husika kama zinavyoruhusiwa na katiba yao kumfukuza huyu Lipumba.
Huu mgogoro wa CCM bara wanaokuza ni Serikali kwa nia tu ya kuisambaratisha CUF/UKAWA. Msajili wa vyama hana haki ya kuingilia mambo ya ndani ya CUF lakini cha kushangaza huyo msajili kaamua kufanya hivyo na kudai yeye anamtambua Propesa Lipumba ambaye alijiuzulu na pia kufukuzwa ndani ya CUF.
CCM KAMWE haiwezi kabisa kukubali kuingiliwa katika mambo yao ya ndani kwa mfano hao waliofukuzwa CCM warudi kinyemela na waruhusiwe kuongeza mfarakano uliopo ndani ya CCM ikiwemo ule wa Wabunge wa CCM kutokuwa na imani na Majaliwa.
Propesa Lipumba ndiye mwenye matatizo hilo halikwepeki hata chembe alijiuzulu na pia kufukuzwa ndani ya chama hivyo si mwanachama halali wa CUF lakini anatumika na hii Serikali dhalimu kuisambaratisha CUF na UKAWA.
Uhuni unaofanywa wa kumtumia Lipumba kufanya fujo ndani ya CUF tena kwa kutumia watu wanaofahamika KAMWE hauwezi kukubalika. Hili likiachwa liendelee linaweza kusababisha maafa makubwa sana kama tuliyoyaona katika uvamizi uliotokea Jumamosi.

Kuna kitu hakizungumzwi sana
ukweli ni kuwa CUF walikuwa na mgogoro wa chini chini wa siku nyingi
kuhusu CUF Zanzibar na CUF bara
UKAWA imetumka tu kuongeza mgogoro hasa kwa CUF bara
kuona CUF Zanzibar wanapora madaraka yoote
Lipumba kaona tu a loop hole la kuwa relevant na kupiga pesa
now kutoka CCM
Solution ni CUF Zanzibar wakubali tu kuwa kuna mgogoro
na wawe ready kuutatua..kuliko kudai tu ni Lipumba ndo mwenye matatizo
Lipumba anapataje support za hadi wabunge?au mtu kama Mnyaa?
tatizo la CUF linazidi kukua now lakini busara ikitumka linaweza kuisha