CUF ni mwiba wa CCM na CDM huku Zenji na malengo yake ni kuikomboa Zenji iwe huru kama ilivokuwa kabla 26April1964,
Baada ya hapo tuna piga stop vyama vingi. Mimi nashangaa Watanganyika mnavyojihangaisha.
CUF haina haja hata ya kiti cha udiwani huko mrima shida yetu ni Zenji tu wacheni porojo zenu. Mtizameni Hamad Rashid ni mtu muhumu lakini hatumuhitaji kwasababu ya kukiuka msingi ya CUF.
Sina shaka na maneno yako, Juzi nimekutana na Jamaa mmoja ambaye mwanzo nilidhani ni mwarabu toka Arabia lakini kumbe ni mwarabu wa Pemba, Mazungumzo yetu yalianza kwa tone ya kwaida na kirafiki kabisa, akaanza kwa kulalamika kwamba anachukia sana kuona Muungano unaifanya Zanzibar kuwa kama mkoa, nikamuambia kwamba Lakini si kuna serikali ya Zanzibar, tone ikabadirika, akawa mkali kweli kweli, pale ofisini kwake kaweka picha ya mwalimu, akaanza kuisonta anasema huyo mzee ndio kaitia zanzibar umasikini huyo, kwa hasira sana akasema, wakati zanzibar inapata uhuru ilikuwa na reserve kubwa sana ya dollar kutokana na biashara ya karafuu, huyo mzee alitumia pesa yote kwenye vita ya IDD Amini, nikamuuliza, kwani wewe haukuona umuhimu wa Tanzania kumfukuza Idd Amini kutoka kwenye Ardhi yake, akaniangaliaaa kisha akasema I do not care, what I know is, if it were not that Mzee Zanzibar ingekuwa Dubai sasa.
Alikuwa amekasirika sana na kwa kuepusha shari Mke wangu akanisihi nisiendelee na hiyo mazungumzo, namshukuru mungu baadae mtoto wake alikuja kuniambia nisimuelewe vibaya baba yake, huwa anahulka ya kuongea kwa asira sana akiwa naexpress kitu, sikujibu kitu pia.
Kitu kimoja nakijua, kama ambavyo Watanzania bara wameamua kuiunga mkono CHADEMA kuindoa CCM madarakani vivyo hivyo watu wa kisiwa cha pemba wameamua kuiunga mkono CUF ili si kuiondoa madarakani CCM pekee bali na kujitoa kabisa katika muungano.
Tatizo, ni kwamba ubaguzi tunaoufanya watanzania Bara dhidi ya CCM unatofauti kubwa sana na ule wa watu wa kisiwa cha Pemba dhidi ya CCM. huu wa kisiwa cha pemba huwa unanifanya nisiiunge mkono dhana ya SAUTI YA UMA.