CUF, Chadema wamshangaa Nape | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF, Chadema wamshangaa Nape

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 29, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Dunstan Bahai

  VYAMA vya Wananchi (CUF) na Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) vimesema vina historia ya kuuchukia ufisadi na kwamba havina sababu ya kutumiwa na
  mtu au kiongozi yoyote katika kufichua mafisadi wote.

  Kauli hiyo ilikuwa ikijibu kauli iliyotolewa na Katibu wa Itikati na Uenezi wa CCM Bw. Nape Nnauye jana kwenye baadhi ya vyombo vya habari.

  Bw. Nnaye alinukuliwa akisema kwamba vyama hivyo vinatumiwa na pia ni mawakala wamafisadi waliomo ndani ya CCM katika kumchafua na kumpaka matope Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.

  Akizungumza na Majira jana, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba, alisema kuwa amestaajabishwa na kauli hiyo ya Bw. Nnauye kwani wao wamekuwa mstari wa mbele na wanayo historia ya kutangaza na kuwafichua mafisadi nchini.

  “Chama chetu kina historia ya kuchukia ufisadi, na tumekuwa mstari wa mbele katika kutangaza sera zetu zikiwemo za kuuchukia ufisadi kama ule wa manunuzi ya
  rada, ndege ya Rais, mikataba mibovu ya madini, EPA, IPTL na ufisadi wa ina yoyote hiyo… na mstaajabu huyu kijana kama kweli ametoa hiyo kauli,” alisema
  Profesa Lipumba.

  Alisema kuwa hakuna kiongozi au mtu yoyote atakayewatumia wao kama chama, kama
  wa kuchafua watu wengine kwani chama chake kinajinadi kwa sera zake na hata masuala ya ufisadi nayo yamo kwenye sera za chama chao.

  Akizungumza kwa niaba ya CHADEMA, Katibu Mtendaji wa chama hicho, Bw. Victor Kimesele alisema kwanza Bw. Nnauye siyo saizi yake na kwamba hiyo kauli ni ya mfa maji.

  “Huyu kwanza siyo saizi yangu, hizo kauli ni za kutapatapa tu kwani Chadema ilipowataja mafisadi haikutumwa wala kutumiwa na mtu na hata huyo Rais Kikwete alikuwemo kwenye orodha ya mafisadi tuliowataja," alisema Bw. Kimesera.

  Huku akiangua kicheko cha kuashiria kuidharau kauli hiyo ya Bw. Nnauye, Bw. Kimesele alisema kuwa Nnauye anaona hodari kuzungumza sana kwenye vyombo vya habari lakini spidi aliyoanza nayo itakwisha.

  Kwa mujibu wa Bw. Kimesele, CHADEMA itaendelea kuwataja mafisadi na itaendelea kuwaeleza wananchi jinsi wanavyoharibu uchumi wa nchi.

  Alisema kwamba wao wenyewe kwa wenyewe wanajuana mafisadi ni wa kina nani na ndiyo hata kwenye vikao vyao wananyoosheana vidole.

  Katibu Mtendaji huyo wa CHADEMA alisisitiza kwamba chama chake ndicho chenye historia ya kutamka hadharani mafisadi na kwamba hata kwenye orodha ya waliyo nayo wamo viongozi wa juu CCM.

  Alisema pamoja na kauli ya Nnauye, lakini wataendelea kuwafichua mafisadi na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano katika kuwajua walipo na wanachokifanya
  katika kuuhujumu uchumi wa Tanzania.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mwacheni dogo atange na njia akikua ataacha!!!!!!!!!! Mtoto siku zote akinunuliwa mdoli siku za mwanzo mwanzo si mnajua tena, hakuna hata watu kunywa maji tena mitaa yote!!!
   
 3. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Nape asingekuwa fidsadi asingalikuwamo kwenye chama hicho. Hana jipya.
   
 4. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,919
  Likes Received: 451
  Trophy Points: 180
  Babu--baba--mtoto--mtoto wake--mjukuu--kitukuu--....hii ndio source ya yeye kuwa huko!!
   
 5. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mmmmhhhh hii kali sasa...
   
 6. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,549
  Likes Received: 4,675
  Trophy Points: 280
  Napy Mwandozya unacheza ngoma ya kitoto na siku zote ngoma yaya kitoto haikeshi.Hakuna chama cha upizani kinachoweza kupokea hiyo mizoga,hao saizi yao huko huko CCM, tunajua mchezo mnao cheza. Kama kweli nyie ni wanaume wa shoka wapelekeni mahakamani na warudishe vijisenti walivyofisadi.Na kama kweli sheria itafuata mkondo, basi na JK lazima awemo kwenye mkumbo wa kwenda jela
   
 7. m

  mkulimamwema Senior Member

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Nape anakera sasa wapinzani wanatetea mafisadi ilihali ccm bado inawahifadhi,amwulize mwenyekiti wake kwanini wasubiri siku 90 hayo ni madhaifu ya mwenyekiti wao.Mwenyekiti wa kweli alikuwa Nyerere na aliondoka na ccm yake safi si hii ya watu walafi wa mali za umma macho yamewatoka na wamejaa fitina
   
 8. T

  Topical JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kabla ya kumshambulia nape mwambie Mbowe arudishe 200 mil. ya Lowassa, na gazeti lake la tanzania daima liache kumsafisha lowassa...

  Ni vizuri chadema wakamchukua kabisa lowassa wakiona anafaa!
   
 9. k

  kimandolo Member

  #9
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tropical, inaonekana sasa uzee unakusumbua kma babu yako makamba, bora ujiengue jf
   
Loading...