CUF bara wamlaumu, wamtega Maalim Seif Sharrif Hamad

Mondoros

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2015
Posts
629
Reaction score
474
Hali ya kisiasa ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) imeendelea kuwa ya utata kufuatia wana-CUF, ambao wengi ni wafuasi wa Mwenyekiti 'aliyefukuzwa' wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba kumtaka Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharrif Hamad kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa chama hicho la sivyo asitarajie kukanyaga kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho yaliyopo Buguruni jijini Dar es Salaam.

Wakiongea katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo eneo la Buguruni jijini Dar es Salaam, wanachama hao ambao wameweka kambi katika ofisi hizo wamesema endapo Maalim ana mapenzi mema na chama hicho anapaswa kumtambua Profesa Lipumba la sivyo ataishia huko huko Zanzibar.

"Huyu Maalim Seif anaiyumbisha sana CUF na amekuwa anafanya hivi kwa miaka. Hadi kufikia hali hii Profesa Lipumba amepitia magumu mengi. Sasa hatukubali kumwona Seif anamburuza Profesa, tumeamua kusimama kwa niaba yake'" alisema Samson Kapilima anayefanya biashara ya kuuza mbao katika maeneo hayo.

Akiongea na mwandishi wa Dar24Media aliyekuwa maeneo hayo, Abdalla Kambi aliyejitambulisha kuwa ni mwanachama mkongwe wa CUF amesema kuwa ili kutuliza hali ya mtafaruku iliyopo katika chama hicho Seif Hamad anatakiwa kuitisha mkutano na kutangaza kumtambua Profesa Lipumba kinyume chake watachukulia kuwa ametimiza azma yake ya miaka miaka ya kuigawa CUF bara na kubaki na CUF Zanzibar.

Mwanachama mwingine wa CUF ambaye alikuwepo katika maeneo ya ofisi hizo za CUF Buguruni, anayejulikana kama Ramadhani Haji maarufu kama " Mzee wa mbende mbende' alimlaumu Seif Sharrif Hamad kuwa daima amekuwa mwepesi wa kuwasaliti na kuwahukumu viongozi wenzake hasa wa upande wa Tanzania Bara.

“Huu mchezo sisi tuliujua miaka mingi maana maalim Seif huwa ana chuki ya wazi sana na watu wa Bara. Alikuwa anamtumia Profesa Lipumba ili kupata uhalali wa Tanzania Bara. Profesa Lipumba ana wafuasi wengi tu Bara na Visiwani na hivyo ana uwezo wa kuanzisha CUF B ambayo itakuwa tayari kushiriki uchaguzi hapo 2020,” alisema Ramadhani Haji.

Wanachama hao wa CUF wamesema wameanzisha umoja wao unaoitwa TWENDE NA PROFESA LIPUMBA ili kumwonyesha Maalim Seif kuwa asiwachukulie rahisi rahisi
 
wana cuf wengi, nazani hujitambui, na kama we si lipumba basi ni watu wake wale wawil anaokaa nao pembeni wakati akiongea na waandishi wa habri...
 
LIPUMBA CCM SI ALISEMA ATASHAURI UCHUMI SERIKALI YA MAGUFURI SI ASHAURI SASA
 
Niliambiwa zamani kuwa si rahisi kung'oa mbuyu
( uliokomaa haswa)na mizizi yake. leo ndio na prove Maalim chukua hiyo.
 
Lipumba kaacha ushauri wa kiuchumi kaamua kuwa mshauri na muandaaji migogoro ya kisiasa kwa maslahi yake
 
CUF wajipange upya kumaliza tofauti zao, otherwise mambo yanazidi kuharibika.
 
hii ni historia inajiandika, mapinduzi haya yanaweza kukirudisha bara ambapo ndio nyumbani halisi kwa cuf ya mapalala iliyopinduliwa na maalim kisha kujengewa ngome nchi ya watu weusi.
 
Acha uongo wamemlaumu wapi? MTU kajiuzulu mwenyewe kapiga Hela kawakimbia wakati wa uchaguzi Leo anarudi eti anauchungu Na chama mnakubali
mkuu. Kunamambo, unaweza yatafakari nchii ukapatwa na ugonjwa wa sotoka.

Mtu ajitoe mwenyewe. Tena wakati chama kipo katika aliyakusaka ushindi! Alafu anakuja na mijitu inashangilia!!!!!

Wangemwuliza swali mojatu kwamba alipokuwa anajitoa alikuwa analengogani?

Je! Chama kingepoteza majimbo yote na kufutika kabisa kwenye ulingo wa kisiasa wangemshangilia?
 
Siasa za bongo zinachekesha sana wakati wa uchaguzi oooh CUF ikishinda Zanzibar muungano ndio byebye sasa hivi sasa yanawatokea mwenyewe baina ya CUF visiwani na CUF bara sasa sijui tuaelewaje??? Acha movie iendelee next episodes au season.
 
Profesa angejitoa once and forall kwanye hizi movements za kuburuzana kama ya ukawa haina maana yoyote kwa upande cuf.
 
Back
Top Bottom