CUF, anzeni sasa kutengeneza na kuandaa mbadala wa Maalim Seif.

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
32,375
29,732
Habari zenu!
Nafikiri ni muda muafaka sasa chama kikuu cha upinzani cha Zanzibar, CUF kujipanga upya. Toka chama hiki kimezaliwa kimekuwa na mgombea urais mmoja upande wa Zanzibar.

Ni lazima kusoma alama za nyakati kuwa huyu mzee sasa HAKUBALIKI na hana jipya. Kibaya zaidi, sijaona vijana wa CUF ambao labda ni toleo jipya la kubeba bendera ya CUF kutoka kwa Maalim Seif.

Endapo mtaendelea kumng'ang'ania Maalim Seif kama ndiye mgombea pekee wa maisha wa CUF, kuna hatari kubwa mkapotea kwenye ramani ya siasa. CCM wamechukua ngome yenu ya Pemba na inategemea watafanya vipi, ingawa siasa za Zanzibar ni za hisia zaidi inapokuja suala la Pemba na Unguja na zinarithishwa kwa vizazi, tukubali kuwa kizazi cha leo kinabadilika. Endapo CCM watafanya vizuri ndani ya hii miaka mitano huko Pemba basi kuna wana CUF watabadili mlengo.

Badala ya kuwa chama cha kutegemea matukio, muda huu ambao 'mpo likizo' JENGENI chama. Tengenezeni vijana wenye kujenga hoja zenye misingi na itakapofika 2020 mumsimamishe mtu mwingine mwenye maono mengine yanayoendana na dunia ya sasa na ijayo.

Maalim Seif abaki mwenyekiti ila asimamie vijana kupewa nafasi zaidi ya uongozi ili baadae waje peperusha bendera ya chama. Wapiga kura wengi ni vijana na hao vijana wa sasa wana upeo wa kudadavua na kuhoji mambo, hivyo ni suala la CUF kuamua kusuka au kunyoa. Chama kipo njia panda!

ANDAENI MTU MWINGINE WA KUGOMBEA URAIS 2020 BADALA YA MAALIM SEIF kuanzia sasa, nasema hivi sababu sioni dalili za Seif kutokugombea 2020. Kuweni na jicho la kuona kesho, sio la kuona leo tu na jana.
 
mzee naona ukatafute chibuku pamoja na bangi ndio utakuwa sawa CCM kwa taarifa yako washatawala Tanzania kwa mabavu miaka hamsini hakuna lolote la lamaana walilofanya zaidi yakuleta njaa, utapia mlo, aids, wizi, ujambazi, rushwa, ujinga, uuwaji, mafuriko,ukame, pamoja na vurugu tupu hujuwi serikari hujuwi lolote ni ujambazi tu.
 
Mi naongelea CUF ya Zanzibar, wee unaongelea ukame bara, wapi na wapi?
Sababu ya upinzani mbovu ndo hivyo ulivyotaja vitaendelea kuwapo, upinzani mbovu ninpamoja na Seif kung'ang'ania kuwa ni LAZIMA siku moja awe rais. Vyama vyenyewe pinzani ndani yao havina demokrasia.
 
Back
Top Bottom