Cry my beloved Tanzania, cry!

Hii issue ya Magufuli leo vyema ikatazamwa kwa upana wake. Hao viongozi wanaowaza ubunge wakati bado wakiwa na vyeo vingine mfano RC ndio wabinafsi, hauwezi kuwaza cheo kingine wakati hapo ulipo una kazi ya kuwafanyia wananchi, hiyo concentration utaito wapi!

Mfano wa Gambo, Magufuli anasema wamekuwa kwenye mgogoro na wenzake kwa miaka miwili, na huu mgogoro umesababishwa zaidi na ujuaji "egoism" ina maana Magufuli aliwapa muda wa kujirekebisha lakini hawakufanya hivyo mpaka alipoamua kuwatumbua, hapa sioni kwanini Magufuli alaumiwe!.

Kwanini wasilaumiwe hao wanaoonesha uroho wa madaraka kwa kuanza kutafuta ulaji mwingine huku wakiwa tayari na kazi ya kufanya mbele yao (kuwatumikia wananchi)? huozo kama huu ndio mnaufunika kwa kuwaita vijana "ambitious".

Hiyo ambitious ingekuwa na maana zaidi kama wasingesababisha migongano na wenzao kwa tamaa zao za kutafuta ulaji mpya, lakini kama ni "ambitious" ya kutengeneza migogoro kwangu naona haina maana, mbaya zaidi ambitious ya kukimbilia mkate mkubwa zaidi (ubunge) huu kwangu ni ulafi wa madaraka, msiutengenezee jina jipya la kistaarabu.

Hapa tusidanganyane, kiongozi wa umma jukumu lake la kwanza ni kuwatumikia wananchi, atimize majukumu yake hapo perfectly ndio baadae awaze kuutaka ubunge, lakini kama anashindwa kutekeleza majukumu yake kwa sababu ya kuuwaza ubunge huo ni ulafi, anastahili kutumbuliwa; na mwishowe Magufuli kasema hata yeye anajua hiyo ndio demokrasia, lakini tusitumie kivuli cha demokrasia kwa kushindwa kutimiza majukumu uliyopewa mwanzo.
 
Siku hizi hakuna cha kustaajabisha kinachotoka kinywani mwa Mwenye nchi yake. Kilichonishangaza leo, ni roho iliniuma kwa niaba ya mamia ya vijana hapa nchini, ambao leo wameambiwa wazi kwa kila namna isipokuwa kwa maneno dhahiri, kuwa hapa nchini kuna anayetoa toa na kutwaa, anayepangia kiasi unachostahili kufikia katika maisha. Mjuaji wa yote. Mungu Mtu. Tuliotaharuki ile siku tuliposikia JINA LAKE LIHIMIDIWE, tulikuwa hatujaelewa somo.

Hivi mtu mwenye mapenzi mema anawezaje kuwaambia vijana wasiwe ambitious?

Kwamba ukiwa Mkurugenzi au Mkuu wa Mkoa, usijaribu kuwa na ndoto ya kuutaka Ubunge au Urais?

Utovu wa nidhamu wa viongozi walioambiwa wakajipe semina elekezi, na wanaoona wenzao wa kanda maalum wakikosa nidhamu ndo wanakingiwa kifua, ni ishu tofauti kabisa na kutishia watu wasijaribu kuota zaidi. Yeye huko kote alikopita alitatua matatizo yote?

Yeye mbona hakuridhika alipoteuliwa na wizara kuwa mwalimu huko Sengerema?

Kwahiyo Masauni, Mwinyi na Mbarawa ndo wasitegemee tena maisha kwenye siasa wakikosa urais Zanzibar?

Vijana wa nchi hii kwakweli wamepatwa.

Mwenyezi Mungu aliyeko mbinguni, awasimamie hiki kikombe nacho kipite. Leo nimethibitisha kwa masikio na macho yangu, kuwa NENO LINAISHI.

Mhubiri 4:3 BHN
Lakini ana heri zaidi kuliko wafu na walio hai, yule ambaye bado hajazaliwa na kuona maovu yote yanayotendwa hapa duniani.
"... yeye mbona hakuridhika alipoteuliwa na wizara kuwa mwalimu huko Sengerema ... "

Kaka mi nafkiri hapa tuchati ...
 
Watanzania chukueni hatua fasta, siyo mnaishia kuandika essays mitandaoni tu.

Hatua gani hizo mkuu?

Mkuu wa jeshi la polisi, mwenye dhamana ya kutuhakikishia usalama = KANDA MAALUM

Mkuu wa Majeshi yote nchini, ´´mwenye uwezo wa kuamua kieleweke na kikaeleweka `` = KANDA MAALUM

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, mwenye dhamana ya kutangaza mshindi/mshindwi = KANDA MAALUM

Mkuu wa watoaji haki mahakamani, jaji mkuu = KANDA MAALUM

Mkuu wa waganga wa kienyeji na wachawi nchini = KANDA MAALUM

Hivi tunapenyea wapi? Hebu toeni mawazo, maana mie upenyo wangu umeishia kwa hizo njia kuu 5 nilizoziorodhesha hapo juu.
 
MZEE MBINAFSI SANA

Kuna siku nimewahi kumtazama rais mstaafu wa hapa kwetu akiwa nje ya nchi akilalamika sana kuwa viongozi wa Africa wanao ubinafsi mkubwa sana. Nilidhani alikuwa anatumia nyumba yake kama mfano halisi! Nilikosea sana!
 
Back
Top Bottom