Cristiano Ronaldo amvisha Pete ya uchumba mpenzi wake Georgina baada ya miaka 9 ya kuwa pamoja

Cristiano Ronaldo amvisha Pete ya uchumba mpenzi wake Georgina baada ya miaka 9 ya kuwa pamoja

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Cristiano Ronaldo amemvisha pete ya uchumba mpenzi wake wa muda mrefu, Georgina Rodriguez. Wawili hao wamekuwa kwenye mahusiano kwa miaka 9 sasa na tayari wana watoto wawili pamoja.

Georgina ameweka picha ikimuonesha akiwa amevalia pete ikiambata na caption isemayo “Yes I Do” akimaanisha amekubali kuolewa na nyota huyo wa Al Nassr ya Saudi Arabia.

1754980273686.png

Thamani ya pete ya uchumba ya Georgina, ambayo amevishwa na Cristiano Ronaldo, inakadiriwa kuwa kati ya Dola milioni 3 (Tsh. 7.5 bilioni) hadi 5 (Tsh. 12.6 bilioni).

Ronaldo na Georgina walianza uhusiano wao mwishoni mwa mwaka 2016 baada ya kukutana katika duka la Gucci, ambapo Georgina alikuwa akifanya kazi kama mhudumu wa mauzo

Wamejenga familia pamoja, wakilea watoto wao Cristiano Jr., mapacha Eva na Mateo, Alana Martina, na Bella.

1754980797544.png
Tunatarajia harusi mojawapo inayotazamwa sana michezoni, ikichanganya soka, mitindo, na hadhira ya kimataifa waliyoifuatilia hadithi yao kwa miaka mingi.
 
Duu kwahiyo kwa miaka yote hadi kupata watoto kumbe bado alikuwa mchumba. Na wazazi wa binti walirizia binti yao kuishi katika hali hiyo au maana mi nilijua ni huku bongo tu kuna uchumba sugu
 
Duu kwahiyo kwa miaka yote hadi kupata watoto kumbe bado alikuwa mchumba. Na wazazi wa binti walirizia binti yao kuishi katika hali hiyo au maana mi nilijua ni huku bongo tu kuna uchumba sugu
Pesa inanguvu sana mkuu
 
Huyo dada hata bila ndoa lakini alishasainishwa mikataba. Huyo mwamba yuko vizuri kwenye hiyo sekta ya uchumi usicheze nae. Ndio maana unaona kuna gold diggers wengine kama Irina Shayk walikimbia
 
Sasa Hata Wewe Ungekuwa Ndio Wazazi Wa Huyo Binti Na Mkwe Ndio Huyo Cr7.....Ungeleta Ngebe..??
😁anafananisha CR7 na akina Fadhil na akina Nurdin wa buza ambao kufungishwa ndoa na akina Mwaju hadi wafumaniwe na kupigwa ndoa ya mkeka, na uhakika wa Mwaju kula Milo miwili japo kwa siku 3 ndoani ni haupo kabisa. CR7 kwilima la dunia, hakuna namna zaidi ya kulivumilia
 
Back
Top Bottom