CRDB Visa Card: Utata wa matumizi yake mtandaoni

Nilishangaa nilipowekewa pesa kwenye CRDB Account na mi nizichukue huku (MAlaysia)
Nikajua kahela kenyewe ka ngama nakuwa naenda ATM kila ninapohitaji, zikatoka poa tuu baada ya kutoa mara mbili tatu naambiwa BAlance haitoshi mhhh nikashtuka
Kuuliza nikaambiwa gharama ya kutumia hii card inakata Malaysian Ringit 140 (USD 40) kwa kila unapotumia hii card hata kwa kuangalia Balance.
Duuuuuh niliishiwa nguvu si unajua dola 40 kwa mwanafunzi tena nyingi sana hizo, Nikaiweka kabatini na siitumii tena.
 

Pole sana mtu wangu ...

Kwa wale washabiki wa kupenda vya nyumbani, utashangaa huyu mwenzetu akipunguza kuvipenda?
 
Ila ukiwa Bongo ukilinganisha CRDB na benki zingine kubwa zenye mtandao mkubwa mikoani na walayani kama NBC na NMB bado nakiri CRDB wana unafuu!

Hivi ulishaenda NBC Co-oporate uangalia huduma? Unakuta wateja 300 na madirisha mawili tu yanafanya kazi! Na NMB yaani foleni balaa!

Mie mteja wa CRDB na NBC...ila kwa huduma pamoja na matatizo yote haya CRDB ni bora zaidi!
 
Hoja hii ilijadiliwa muda mrefu uliopita nadhani hoja ya mwisho ilitolewa Machi 2009, Na mimi ni mara ya kwanza kuingia katika jamvi hili la JF, nilifuatilia thread hii kwa makini sana,
Sasa na nina mpango wa kutafuta visa card ili niitumie kwenye mtandao maana kuna programu moja ambayo iko mtandao ambayo natakiwa kuinunua na gharama yake ni Dola takribani $90. Na jinsi ya kuipata au kui-dwnload inatakiwa nitumie Visa Card. Lakini kabla ya wazo hilo la Visa card nikaamua kutembea Jamvi hili na ndipo nikafanikiwa kuona mjadala huu.
Kwa kuwa wazo langu la kupata programu hiyo liko palepale, Nakusudia kuwa na kadi mbili, moja ni kwa ajili ya kuhifadhi tushilingi twangu na nyingine iwe maalumu kwa mtandao. Kwa mfano katika kadi hii ya mtandao naweka kiasi kile tu kinachohitajika katika manunuzi yangu.
Maswali: Je hawa CRDB bado kuna kale kamchezo kama ilivyochangiwa na wanaJF mbalimbali? hasa kuhusu usumbufu wa kupata statement.
Na wizi wa pesa mtandaoni bado haujadhibitiwa?
Na je kuna marekebisho yoyote yaliyofanyika na CRDB kuhusu kale kamkataba ka kuiruhusu card itumike kwenye mtandaoni?

Waheshimiwa naomba kutoa hoja,
 
Mbona mwanzilishaji wa mada hii ana mambo ya kizamani, every who engages in having a visa card with is online active should expect to encounter such risk. cha msingi ni kujua what are the risks involved basi and the be careful. another important factor is to know the safe sites on the internet. Stop being a bigot and embrace technology.
 
Ndugu ni kitu gani hicho unachotaka kununua ambacho tanzania hakuna ? Naomba unifahamishe naweza kukuelekeza duka wanalouza au kampuni inayo deal na programu hiyo

ahsante
 
Ni programu ya music inaitwa Notation Composer Software, nadhani wale wanaofahamu mambo ya do re mi fa so la ti do wanafahamu, kama wana taarifa zaidi au wapi inapatikana wanijulishe
 

Asante kwa mchango wako mzuri, na hongera kwa kufanikiwa ku-embrace technology. Sisi wengine utatusamehe, upeo mdogo.

Bigot maana yake ni nini tena?

Anyways, mimi nilidhani tulichojaribu kufanya hapa ni kuwaambia watu "what are the risks involved basi". Kama unadhani hilo ni kosa, basi samahani. Tungeomba labda utuelekeze njia ambazo watu wanaweza kutumia kutambua hizo risks involved.
 
Last edited:
Nashukuru, kunipa hiyo link, tatizo langu ni jinsi ya kuinunua ili niweze kuitumia kwa muda mrefu nitakao. Programu nilishai-download trial version ya siku 30, ambazo tayari zilisha-expire. na nikijaribu mara ya pili inagoma mpaka niinunue. na gharama yake ni USD 87.99.
 
Niliyoweka hapo sijawahi kuitumia. Hata hivyo, ni matarajio yangu kwamba utaweza kuitumia kwa zaidi ya siku 30.

Nimeeleza kidogo (post no. 443) kuwataka watu wachukue tahadhari pale wanapo-install software za namna hii from unknown sources.
 

Mkuu,

Ahsante kwa maelezo yako ambayo kidogo yamenipa mwanga kuona kwamba bado Tanzania hakuna mfumo wa maana wa ulipaji fwedha mtandaoni au electronic payment system kama unavyojulikana.

Kwa sisi tulio nje ya Tanzania si tu kwamba tumezoea mfumo huu, bali pia hata aina zingine za malipo kama mobile payments, digital payments, e-cash na e-cheques.

Wafanyabiashara wote duniani wakiwemo mabenki ambao hutumia electronic payment system katika internet wanaitwa merchants na wako liable kwa wale watoaji wa kadi hizo zenye nembo ya VISA na MASTERCARD.

Mara nyingi wakishindwa kufikia viwango vinavyokubalika kimataifa basi hutumia third parties kama PayPal na kadhalika ambao kumalizia taratibu zote za malipo kwenye internet kwa niaba ya mteja, hawa wanaitwa Payment Service Providers.

CVN (card verification number)

"Merchants" wote wakiwemo CRDB ni lazima wazingatie kanuni na taratibu zote za kuhakikisha kwamba malipo yanayofanywa na mwenye kadi ni kutoka kwake yeye mwenye kadi.

Hii ni pamoja na kuweka security protocal ( hapa kuna mambo mengi kama CGI au (common gateway interface) na hatua zingine za kuhakikisha kadi inatoka mahala sahihi vikiwemo certificate of authorization na mfumo wa PKI au public key infrastructure ambao unatoa kinga kwa kila transaction inayofanyika kwenye internet.

Ikiwa CRDB bado hawajafanya hivi basi huu ni ujinga wa hali ya juu.

Njia ya pekee kwa sasa ambayo ni salama ni kwa watu kutumia PayPal kwa any transaction.

Halafu mkuu umeongelea juu ya kufananisha anuani ya mteja anaefanya transaction online kama inafanana na anuani ambayo imo katika kadi ya mteja. Kama CRDB wameminya kama unavyosema huu ni uvunjwaji wa kanuni za kibenki na kibiashara labda kama mpaka sasa Tanzania hatuna public address systems ambapo mtu anaweza kupata mzigo wake baada ya kuununua.

Public address system ni rahisi sana kuiunda endapo pana nia ya kufanya hivyo na uundwaji wake unaweza kuchukuliwa simple tu kwa kuangalia motherboard ya computer jinsi ilivyoundwa, na hii ndio utapata system nzuri ya kutuma na kupokea barua na mizigo.
 
Last edited:
Nakubaliana, technolojia hii bado haitusaidii.
 
Duuh...hii taarifa muhimu sana kwangu maana nilianza mchakato wa kujisajili na tayari nilishaanza kuweka dau kwenye mnada wa ebay. Yaani hii nchi kila sehemu ubabaishaji hata tunakoweka amana zetu nako hovyo asa tuende wapi?? Sio siri nchi inachosha kweli hii yaani kama tupo vikumbulu ama kimazichana bwana. Ahsante mdau kwa taarifa
 
Ndugu Manitoba na wanajamii FOrums wengine.

Msiogope kutumia VISA Electron debit card.

Jawabu: Jisajili paypal.com na utaweza kununua huduma kwenye internet bila namba za kadi yako kujulikana
 
Ndugu Manitoba na wanajamii FOrums wengine.

Msiogope kutumia VISA Electron debit card.

Jawabu: Jisajili paypal.com na utaweza kununua huduma kwenye internet bila namba za kadi yako kujulikana

Sadakta!

Ndio tunachowaambia watu hapa, unless unajua unachokifanya, jaribu kuepuka kutumia kadi yako moja-kwa moja. Na paypal inaweza kusaidia kufanya hivyo.

Mimi mwenyewe nimeiweka hiyo kadi papal, natumia paypal badala ya kutmia kadi moja kwa moja.
 
Mimi mwenyewe nimeiweka hiyo kadi papal, natumia paypal badala ya kutmia kadi moja kwa moja.
Hili ndilo wazo ninalokusudia kulifanya. Asante kwa ushauri wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…