CRDB tangu asubuhi hakuna huduma

Nilidhani kwangu tu maana toka saa nne nahangaikia kutoa pesa ,
 
Hiyo bank Kuna vitu vinaendelea ndani kwa ndani wateja hawavijui... Haiwezekani kila wakati Kuna series ya malalamiko ..
 
Wanakera wajinga hawa, wanapoteza muda wa watu bila sababu za msingi.
Yani imenibidi nifunge safari nirudi mkoa mwingn kufata cheque kisa ujinga wao..

Kama hawawez huduma wafunge hiyo benki
Ni kwa matawi yote au tawi moja? Lakini suala la kukosekana kwa mtandao (network ) ni jambo la kawaida maana ni la kiufundi zaidi
 
Ni kwa matawi yote au tawi moja? Lakini suala la kukosekana kwa mtandao (network ) ni jambo la kawaida maana ni la kiufundi zaidi
Nadhani ni matawi yote na system yao yote kiujumla , atm ,Sim banking zote hamna kitu , halafu lazima tuwe smart tatizo la netwwok kukata muda mwingi kinakuwa ni uzembe wa watu asilimia chache ndio unaweza kusema ni mfumo wenyewe, halafu hakuna fail safe kwenye mtandao ya kibongo , atm Sim banking na hata wale wa counter inaonekana at some point wanatumia source moja , mafhara yake ndio hayo vitu vinafail kwa pamoja
 
Ni kwa matawi yote au tawi moja? Lakini suala la kukosekana kwa mtandao (network ) ni jambo la kawaida maana ni la kiufundi zaidi
Kwa kila tawi, benki gani inasumbua network nchi nzima?
Mbn benk zingn hakuna huu ujinga?

Halaf kwa network kushindwa kunaleta usumbufu na garama ambazo sizo.

Imagine nimesubir malipo kuanzia jumamos hadi saiv sijapewa na benk zinafungwa saa kumi hii, boss anasema nifate cheque yye hasubir network..sasa fikiria nimetoka mkoa mmoja nimeenda mkoa mwingn kisa huu ujinga wao..shit!
 
Nadhani huyu CEO mpya kazi imemshinda

Nimeenda Holland House mara tatu nawauliza kuna tatizo gani wanasema hata wao hawajui ni issue ya system. Yaani hela yangu kuweka kwenu ndio mateso, basi muwe hata na lugha ya staha kwa wateja hata radhi hawaombi. Nimekwama kulipia ununuzi wa bidhaa mtandaoni nilipewa discount ya USD 400 nilipie ndani ya saa 1 nimeshindwa. Wameniboa sana, Imagine una mgonjwa labda anahitaji hela atibiwe si anakufa kwa ujinga wa hii benki.

Enzi za Dr. Kimei hakukuwa na huu utopolo, ili jamaa la sasa hivi linaua benki
 
Yaaani
Ndiyo naahituka mchana kuhusu hili tatizo. Umuhimu wa kuwa na akaunti 2 sehemu tofauti. Gharama ya kuzimiliki bado zina ku save kipindi kama hiki. Duh
 
Mimi nimekaa Benki kwa muda wa masaa mawili nikisubiri kitu kinaitwa network.
 
Si huwa mnatudharau sisi wenye account bank nyingine..haya sasa,leo mmeipata fresh.
 
Back
Top Bottom