Selwa
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 671
- 699
Basi katika pita pita zangu nilikuwa mkoa flani weekend ya mwisho mwezi wa tano. Si unajua mambo ya furahi day nikaenda atm kutoa fedha nianze kuleta fujo mjini maana nilikuwa hata bati sina. Mimi ni mteja wa crdb so Nikaenda karibia ATM zao 3 mji mzima hazina network. kwa takribani maasaa 6. He... basi nikaona hebu nijaribu kutoa atm ya benki nyingine ya VISA. mdogo mdogo nikaenda NBC sasa baada ya kuweka kadi atm ikaandika 'Issuer not available' nikajua labda tatizo ni CRDB yenyewe ndo mana nikatulia nikarudi zangu home. hata dakika hazijapita niko njiani ikanijia messeji umetoa laki sita frm XXXX ATM. Heeee! mbona haikutoa hela? nikarudi ile atm na kweli ipo empty na sioni pesa yeyote nikamuuuliza mlinzi akasema inatokeaga ni mtandao piga hiyo namba kwenye msg (nilipiga ila haikupokelewa) basi kwasababu muda wa kazi ulikuwa ushapita nikaenda kesho yake kuripoti. Nikaandika details kiasi chenyewe, laki 6, Baada ya hapo ikawa ni kila siku kufuatilia ka miezi 6 napigwa tarehe tu . Mpaka meneja nikaenda kumwona wapiiiii. nimekuja kupewa jibu juzi kwamba Visa wameshindwa kunirudishia hizo hela kwasababu eti inaonekana nilizichukua? nikauliza imeonekana wapi??? mule kwenye atm hamna camera? maana kweli kwenye acount ilisema hela nimetoa wakati ile atm ilisema issuer not available.kibaya ilikuwa haina risiti!! nikawauliza hamuwezi angalia kwenye camera zao za security hao nbc au hata kuwaomba maana mimi ni mteja wenu na hio ni pesa yngu? wakasema hawawezi! nikabaki nimeduwaaa. laki sita mshahara wa mtu huo. lakini hamna shida. nimeamua kuhama tu benki na nawapa tahadhari na wenzangu kuhusu CRDB na VISA. me naona heri nihame benki tu. Mmezidi wizi.