CRDB jirekebisheni

CRDB jirekebisheni

Capital

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Posts
1,494
Reaction score
1,080
CRDB bank inayojinasibu kumjali mteja kutoa huduma za hovyo. ATMs kuzima muda mwingi hasa kuanzia jioni na mtandao wa sim banking kukosa maana.

Kuna tofauti gani kati ya kuwa na atm au simu au internet na ile "passbook".

Tafadhali jirekebisheni kabla hatujaenda KCB. Mnaboronga wenyewe kisha mnakuja kulia lia , mara oh, serikali hailindi wawekezaji wa ndani.
 
Jani mkuu fatatilia taasisi za mikopo hazikuja kusaidia zimekuja kunyonya watu riba kubwa
 
Huu ni upuuzi crdb bank inayojinasibu kumjali mteja kutoa huduma za hovyo. ATMs kuzima muda mwingi hasa kuanzia jioni na mtandao wa sim banking kukosa maana. Kuna tofauti gani kati ya kuwa na atm au simu au internet na ile "passbook".. tafadhali jirekebisheni kabla hatujaenda kcb. Mnaboronga wenyewe kisha mnakuja kulia lia , mara oh, serikali hailindi wawekezaji wa ndani, oovyoo!
Huu ni ukweli mtupu, CRDB hebu fuatilieni na mrekebishe hali hiyo, msitudharau sisi ni wateja wenu.
 
Huu ni upuuzi crdb bank inayojinasibu kumjali mteja kutoa huduma za hovyo. ATMs kuzima muda mwingi hasa kuanzia jioni na mtandao wa sim banking kukosa maana. Kuna tofauti gani kati ya kuwa na atm au simu au internet na ile "passbook".. tafadhali jirekebisheni kabla hatujaenda kcb. Mnaboronga wenyewe kisha mnakuja kulia lia , mara oh, serikali hailindi wawekezaji wa ndani, oovyoo!

Simu banking cheche bado ukicheck salio wanalamba hela na salio hupati, halafu ndo mwisho wa mwezi munatusababishia jam ofisini.
 
MI Nina milioni moja nimehamisha toka mpesa kwenda bank Ina wiki sasa haijafika
 
Dalili za kufa kwa biashara ni pale mfanyabiashara anapoanza kupuuza malalamiko ya wateja. Huduma za sim banking, visa, internet banking ni ghali na badala ya kuwa msaada kwa mteja zinakuwa msalaba. Potelea mbali gharama, bora zingekuwa za kuaminika... unaweza ukashinda siku nzima bila kupata huduma mbali na kuwepo options zote hizo.. nasisitiza tena.. CRDB bank mnaboa sana.. jirekebisheni
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom