CRDB - Dodoma Badilikeni

Q-liner

JF-Expert Member
Nov 4, 2017
345
636
Lengo la Uzi huu ni kutoa kasoro kwa baadhi ya mapungufu machache kati ya mengi niliyoyaona CRDB- Dodoma.

Haya nimeyaona hususani katika matawi ya Mazengo na Chamwino yote yaliyo Jiji la Dodoma.

Mathalani moja ya kasoro ya mara kwa mara ni Teller anatumia muda mwingi sana kukuhudumia tofauti na Benki nyingine,kumbe ukiangalia kwa makini anachofanya -:

anakusubirisha wewe bila sababu ya msingi huku kuna fomu nyingine za wateja ambazo zimeletwa nyuma ya pazia na wahudumu wenzake wanaanza kuzishughulikia.

Sasa machoni kwa wateja wengine inaonekana we ndo unatumia muda mwingi kumbe kuna baadhi ya watumishi wanawapa kipaumbele baadhi ya watu wanaowajua bila kuzingatia muda.

La pili ambalo limenishangaza sana.

Baada ya kupewa karatasi ya huduma(nadhani wengi wenu mnafahamh utaratibu huu pindi uingiapo Crdb).

Nilikwenda Kwa Teller anaepaswa kunihudumia nilipofika tu akaniambia si unatoka kutoa hela,hapa nimeishiwa subiri nimuhudumie Fulani tena akamnyooshea na kidole kwamba anaweka pesa.

Then akishaweka ndo atanihudumia,ilinibid nikakae nisubiri! Baada ya kusikia maongezi dirishani nikajua kwamba kumbe ulikuwa mchezo tu,ni watu wanaofahamiana hivyo akapewa kipaumbele.

Kwa kweli sikuweza kuvumilia nikachukua maamuzi ya kuondoka, kutokana niliona ni ubabaishaji. Hayo ni machache tu kati ya mengi niliyoyaona ya kibabsishaji kwenye Matawi ya Benki hii.

Ninachowaomba tu badilikeni maana kwa sasa ushindani wa biashara ni mkubwa Afya ya Benki hii mkiendelea hivi itaondoka.
 
Huduma za Crdb hasa matawi ya Dodoma ni sifuri
Niliendaga nataka mkopo wa biashara, nikaona kiwingu tu blaablaa nyingi wakati nimebeba kila kitu
Nikawa tema nikaingia NMB siku hiyo hiyo tukaenda site visit na maafisa mikopo nikasubiri siku mbili nikapewa hela

Kuna hawa Crdb kuna na Equity(Wana watu wao, ambao wanapewa huduma fasta hasa wafanya biashara wakubwa)
 
Back
Top Bottom