Nikiwa mjini Bujumbura niliiishiwa na fedha za kigeni na hivyo kuwa na shida ya kubadili takribani shillingi millioni 2 za Tanzania nilizokuwa nimebakiwa nazo mfukoni ili nipewe ama AMARUNDI au Dollar ili niweze kuendelea na maisha.Baada ya kuzungukia bureau kadhaa amabako walikataa fedha za Tanzania nilishauriwa niende kwenye benki ya CRDB kwani wana tawi kubwa katikati ya Bujumbura.I was shocked nilipoambiwa na ma teller ambao wote ni madada wa kirundi kuwa hawachukui fedha za Tanzania,nilisikia aibu na fedhea kubwa kuona benki ya Kitanzania ikikataa kupokea fedha za kitanzania,jamaa yangu aliyenisindikiza ambaye naye ni raia wa Burundi pia hakuamini alichokisikia,alifedheeka na kunishauri kuwa nitafute mtu anayeenda mpakani wa Tanzania na Burundi eneo laManyovu ili nikabadili kwa vijana wanaofanya hiyo baishara pale mpakani[black market]ndivyo nilivyofanya na jioni nikaletewa hela yangu japo rate ilikuwa mbovu sana.
Swali la kujiuliza je ni kwanini CRDB wanakataa kupokea fedha za Kitanzania,hata kama ni nje ya nchi?Pia customer service inaelekea ni mbovu kwani wale wahudumu wa Kirundi pale CRDB ni tofauti sana na wahudumu katika matawi ya Tanzania.