Crdb banking online | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Crdb banking online

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Dedii, Oct 28, 2010.

 1. D

  Dedii Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 76
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Wadau mm nimteja wa hii bank kwa muda sasa, wanahuduma moja ya banking online, kwakweli nilivyoiona ktk matangazo yao nilipenda sana, hadha ya kupanga foleni itakwisha.. tena haijalishi uko dunia ipi muh imu uwe na conection ya internet.. tatizo nikifungua website yao nikienda ktk option ya hiyo huduma kinachofunguka ni saver timeout. naomba msaada kwa wanaojua namna ya kutumia hii huduma au labda hawana hii huduma?.
   
 2. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,788
  Likes Received: 6,294
  Trophy Points: 280
  Huwa inafunguka vizuri tu, labda kwa sasa wana tatizo la mtandao.

  Huduma hii ya internet banking wanayo. Mimi ni mteja wao na naitumia sana tu. Kujiunga ni lazima uende mwenyewe kwenye tawi lolote la CRDB. Huwezi kujiunga online
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hata mimi nilihitaji hii huduma nikaambiwa kuwa lazima uende kwenye tawi lao na kujaza form. Ila wanatoa huduma mbili tofauti ambazo ni online banking na nyingine nadhani wanaita internet banking (sina hakika). Mojawapo inakuruhusu kuingia kwenye account yako kutokea kwenye website yao na kufanya transactions ila nyingine inakuruhudu kutumia kadi yako kununua vitu online. Ni muhimu kwenda CRDB ili wakufafanulie. Mimi sikuwa na muda wa kutosha kwa hiyo nilishindwa kujiandikisha.
   
 4. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,788
  Likes Received: 6,294
  Trophy Points: 280
  Huduma ya ''internet banking'' inakuwezesha kuaccess account yako kupitia internet. Yaani ukishaingia kwenye website ya CRDB, kuna jinsi ya kulog in.

  Kwa huduma hii, unaweza kuangalia balance yako, transactions tofauti ulizofanya (debit/credit), kumtumia mtu pesa mwenye account na CRDB bank na pia kumtumia pesa mtu mwenye account na bank nyingine - japo kwa huduma hii huwezi kufanya mwenyewe chap chap, inabidi uwatumie message CRDB (wenyewe wanaiita secured message) na wao ndo watafanya transfer siku wakijisikia, unless uwapigie simu.

  Hiyo nyingine unayoiita ''online'' haipo as such ila ni matumizi ya VISA card ya kawaida kabisa kwa bank za wenzetu unyamwezini. Yaani kama una VISA card ya CRDB, unaweza kuwatembelea CRDB (tawi lolote? not sure) na ukawaomba wakuruhusu kuweza kufanya shopping ONLINE. Kuna limit flani ya pesa wanayokuingizia kwenye mpango huo na ukiimaliza, unawatembelea tena ili wakuwekee tena.

  So far, internet banking ya CRDB imetusaidia sisi tulio mbali na home. Ipo fast kiukweli na ukituma pesa online, wanafanya transfer faster.
   
 5. mzozaji

  mzozaji JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2010
  Joined: Jul 28, 2010
  Messages: 257
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mimi naitumia muda mrefu sana kufungua site haina shida kabisa ila transfer nimefanya mara nne imenikubalia mara moja tuu.
   
 6. mzozaji

  mzozaji JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2010
  Joined: Jul 28, 2010
  Messages: 257
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kutumia Visa card yako kufanya manunuzi online sio lazima huende kwenye site , una-swipe tuu kadi yako dukani au unaweka namba online.
   
Loading...