COVID-19 health alerts: US Embassy Dar es Salaam

Kila mtu anaweza kusema lake. Ila tusijitoe ufahamu na naelewa kabisa walioko humu JF ni waelewa lakini utashangaa mabandiko yanayokekwa humu!
Hebu jiulize US ina majimbo mangapi kulinganisha na TZ! Majimbo 3 tu yanaweza kuwa ndio TZ yote. !
Vipimo vinavyofanywa US ni majimbo yote na taarifa zinaletwa mezani kila siku asubuhi na jioni. Ziko timu kila mji zimeundwa na zinatoa taarifa ya vipimo, maambikizi na vifo.
Yanayotokea hapa TZ ni picha gizani. Na pia tuelewe kitengo kikubwa na CDC kina ofisi jiji Dar na wapo wafanyakazi pande zote mbili wa US na TZ. Hivi yanayoendelea ina maana hawayaoni? Hivyo tusijitoe ufahamu ni swala la muda na siasa kuwekwa kando. Wahusika warudi mezani. Hata bunge wanaposema waliosusia vikao waje na barua ya vipimo ni mshangao wataenda kupima wapi wakati hakuna vipimo vinavyosema ukweli!??
Je ni mikoa mingapi inavipimo??
Maswali ni mengi majibu yatasomeka.
Vipi shule zimefunguliwa au watoto wako huko mitaani tu bila Barakoa?

Nnnn.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuindesha nchi kubwa Kama Marekani bila unafiq haiwezekani.Wao Wana maanisha Tanzania ina vifo vingi na wagonjwa wengi kuliko
Marekani,ndio maana Wana wahimiza raia wao waliobaki waondoke. Ubalozi wao ulisha wakodia ndege wakaondoka sasa walioamua kubaki wao binafsi waliona Tanzania ni sehemu salama kuliko kwao. Hivi sasa wanajaribu kulazimisha/ kuwatisha waliobaki ilinao waingie

Sent using Jamii Forums mobile app
Umesoma vizuri lakini ndugu yangu ama lugha imekupiga chenga. Wao wametoa tahadhari kwa raia wao. Wametimiza wajibu wao kama ubalozi. Sioni kama kuna tatizo hapo
 
Wale ambao wanauwezo wa kufanya kazi wakiwa majumbani kwao kwa mfumo wa kimtandao kama rais hawana haja ya kutoka, hata Rais hana sababu ya kutoka maana anaweza fanya kazi kwa video conferencing, sio nesi yule, hawa ndio wataalam wanasema wasitoke maana hawana hajanya kutoka, wengine tutoke kwa sababu tuna ulazima wa kutoka.

Yeye sio kwamba hajatoka tu bali amekimbia ikulu na kwenda kujificha chato
 
Ni ajabu, Jenerali anayejificha huku akiwaamuru wapiganaji wake wasonge mbele kwenye uwanja wa mapambano.

Inaonyesha maambuki ya Covid kuzidi kumeifanya hii serikali iache kutoa updates za màambukizi mapya, lkn watafaulu kuficha? Vifo vitawaumbua.
 
Kama kupishana misimamo ni ujinga.
Hata mimi kwa upande wangu na kuona ni mjinga.
Maana haupo upande wangu..
Unacho kiasi gani cha kunilipa nikupe drasa hapa, hata kama najua ujinga unakulemea sana.
Ujinga na upumbavu vikichanganyika matokeo yake ndiyo haya.

Mtu na akili zako unashinda kwenye mtandao ukijivunia ujinga?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom