Cover Price ya "Majeruhi wa Mapenzi" ni 18,000!!! Book store wanataka 40% 'ngombe wa maskini'...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Kitabu kitakuja na cover price ya 18,000; mojawapo ya maduka makubwa nchini ambayo tumeomba tuweze kuuza wao wanataka 40% ya cover price! hii ni sawa na 7200Ths. Angalia:

Gharama ya kuchapa kitabu kimoja ni 7900Tsh
Gharama ya kusafirisha kwa kila kitabu 500Tsh
Gharama ya duka la vitabu 7200Tsh
Kumlipa msaidizi wangu kwa kusimamia mauzo kwa kila kitabu 1000Tsh
Matangazo ya biashara 2 kwenye magazeti tofauti 700 per book

Jumla ya gharma ya kukifikisha hiki kitabu ni 17,300!!!

Vinginevyo wao wanunue kwenye wholesale na kuuza kwa bei yao

gademu!!!! Kweli anayetaka cha uvunguni sharti ainue kitanda!
 
Hivi ulikuwa hujafanya utafiti kabla?

Wenzenu wanaongea na wataalaam wenye uzoefu sio mnaingia kichwa kichwa tu.
 
Tatizo la Watanzania ni kukurupuka, kila kitu wanajifanya wao wanajuwa. Umekurupuka, rudi uonane na waandishi wa vitabu wenye uzoefu wakupe darsa, muone Mzee Adam Shafi akupe darsa kidogo upate muelekeo.

Unafikiri vitabu unavyiingiza tu sokoni kama unavyoingiza udaku wako kwenye mitandao?
 
Na Ndio maana hata waandika vitabu wamekatatamaa ya kuandika vitabu, gharama kubwa na fedha zote anachukua muuzaji na si mtunzi. Taifa la wajinga Litaangamia kwa Kukosa Maarifa

I wonder kama mfumo huu umewekwa kwa makusudi;matokeo yake tunaingiza hadi vitabu vya hadithi; watoto wetu wanajifunza masimulizi ya watu wengine.
 
Pengine itakuwa cheaper kuchapishia china ama india! Hivi hamna distributors wachina? Jamaa wa XS marketing (sina hakika na jina, wale wana vijana wao wa kuuza hotpot) wanaweza kuwa wazuri. Ngoja nitakuulizia. Uzikate tamaa baba, ndo nchi yako hii umekabidhi kwa wanyang'anyi na wewe hutaki kurudi uwe kiongozi. Yalee ya kamisheni ya kuuza rada!
 
Nimekatishwa tamaa sana! Kama hali ni hiyo kwa MM sijui kwangu itakuwa je... Hata hivyo ngoja tusubiri revolution ulosema pengine itaturudisha kwenye mstari..
 
Back
Top Bottom