hassan mdidi
JF-Expert Member
- Apr 13, 2014
- 421
- 167
Ukiona hivo ujue ndalichako na raisi wake wamefanikiwa katika mpango wao wa kupunguza wanafunzi vyuo vikuu ili kupunguza matumizi ya hela za serikali
JE, ATHARI YAKE NI NINI KWA TAIFA BAADAE?Kweli Ndalichako anafaya kazi yake ameyodhamiria,wangepunguza ada kwa kada za diploma ili basi wakasome huko watu wengi.Lakini kwa hali hii.
tanzania ya viwanda inaelekea kuwa na waandisi wachacheJE, ATHARI YAKE NI NINI KWA TAIFA BAADAE?
Mkuu hili linafaida gani au hasara gani kwa taifa?.
Mkuu ni hatari sana ila trend kwa arts bila shaka itakuwa ya kawaida(sina uhakika),ila kwa sayasnsi kama hali hii ikiendelea basi serikali iangalie njia mbadala yakuongeza wasomi wa science.Nafikiri ni vizuri kupata data za courseprogram tofauti science na arts tuone trend. Kuna programs za vyuo ambavyo viko mbali na Dar sielewi kinacho endelea unakuta mpaka leo program unayofikiria ni nzuri applicants (priority 1 to 5) hawafiki 20.
Hivi wa national service wameshaomba au bado?
Hawajaweka dedline TCU.hivi dedline ni lin wakubwa
Angalia hio atachment baadhi ya course nimeweka nawaombaji wa course husika.we umejuaje
Thank you kwa mchango wako mkuu.Kwa uelewa wangu nahisi hivi,
Faida1, kwakuwa wameongeza vigezo vya kujiunga vyuo vikuu basi lengo lao itakuwa ni kupata wahitimu wachache na wenye kuimudu vizuri taaluma yao na kuipenda pia, zamani mtu alikuwa anaweza enda kusomea kitu kingine kwakuwa nafasi zimejaa na hatimae anakuwa hana uzalendo na hiyo taaluma, hii ni faida kwa serikali ambayo inadai itakuwa ya viwanda kwakuwa itakuwa inapata watu sahihi
Faida 2, kwakuwa pesa zinazotumika kusomesha wanafunzi vyuo vikuu waga ni nyingi mno na mwisho wake serikali waga haina mpango dhabiti wa kuipata kutoka kwa wadaiwa (mikopo) kwakuwa wengi wao waga hawapati ajira hivo serikali inakuwa km inakula hasara hivo kwa kupunguza wasomi vyuo vikuu serikali kuna hela zitakuwa zinabaki hivo nahisi zitatumika katika ujenzi wa taifa katika nyanja tofauti tofauti, km vile kuongeza fursa za kazi na kuwaajili wale ambao hawakupata kazi ila walitumia mkopo na hatimae kukatwa mkopo waliotumia vyuoni
Hasara, sidhani kama Nchi yetu ina wasomi wa kutosha kukidhi mahitaji ya nchi sasa unapoongeza vigezo kwa nia ya kupunguza wasomi ilhali bado mnawahitaji matokeo yake sijui ile issue ya kutoa wataalamu rwanda itakuwa endelevu
Hasara, kwa nionavyo nahisi wasomi wengi watakuwa na hasira na serikali na hii kupelekea wengi wao kufanya kazi bila morali kwakuwa wafanyakazi wengi wa serikali ukiacha nafasi zao za juu yani ukurugenzi kupanda juu, waliochini ya hapo % kubwa wana elimu ya diploma sasa mtu alikuwa na nia ya kujiendeleza na alisoma kipindi GPA inahitajika 2.7 na leo imepaa hadi 3.5 na wapo wachache ambao wanazo hiyo GPA ila wanakuja kufungwa na issue ya ukienda kusoma hupati salary ss kwa mishahara yetu ya serikali ilivo ni wachache wataweza kwenda kusoma na kuacha mshahara, hapo razima huyu mtu ajenge chuki kwakuwa malengo yake yamekufa hivo ataona km atadharaulika sana, hii itapelekea wasomi pamoja na wafanyakazi kutafuta kazi katika mashirika binafsi au kutoka kabisa nchini na kwenda kutafuta kazi nchi za jirani
Sasa mkuu huko sekta ya afya kama wapo wengi sindio itakuwa balaa,kama Udom,st francis,imtu wamevifungia.Itabidi hao wanafunzi waaply mwakani.Upepo umehamia sekta ya afya watu wanaosoma pcm advance si wengi kama wanaosoma cbg na pcb ambao wote hukimbilia kusoma afya
Bila shaka unazungumzia uhadisi wa majengo na barabala,mbona siwaoni wahandisi wachina katika umeme,mitambo,maji ,mawasiliano,kemikali,mazingira,n.k?Ha ha ha ha ha! Mkuu Unauliza Swali ambalo Jibu Lake Lipo Wazi!!!!!
Katika Uhandisi Kazi Zote Wanapewa WACHINA sasa nani atasomea Uenjenia???!
Kama Huamini Ziangalie Fake Kampuni Za Wachina Zinavyopiga Dili hapa tz.
Yaa inawezekana vipaumbele vya serikali vimebadilika katika elimu.Sio kupata tena wanasansi wengi Bali wasomi wengi?.Mwaka huu tegemeeni kuona wanafunzi wachache katika masomo yanayohusiana na sayansi ila vyuo vikuu vitajaza wanafunzi wa program za art. Ukiwa na viongozi wasiojua kwa muda gani kunahitajika nini, hilo taifa haliwezi kuendelea.
Wangeboresha zaidi vyuo vya diploma huko watu ndio wakaenda kusoma bure.Serikali ya Magufuli imekuja na sera ya ajabu sana japo haijaandikwa. Huwezi kuzuia watu kupata maarifa ukategemea kufaulu.
Sawa mkuu,mimi nmemuombea dogo tu ila umeweka mchango mzuri thanks mkuu.kuna wakati system ya tcu huwa haijiupdate, ilitokea mwaka jana namba halisi ya walioomba ilionekana baada ya deadline ndo mtu anashtuka kukuta waombe 200 wakati ye alijua ni 100 na kwa wakati huo hana option tena, so kuwa makini ukiona namba hazichange