Habari wana jamii,
Nina jambo ningependa kujuzwa kuhusu hizi namba za kupiga simu za nchi tofauti tofauti.
Kwa wanaofahamu ukitaka kupiga simu nje ya nchi kama Marekani lazima uanze na +1 kisa namba ya unaempigia hivo hivo hapo kwetu ni +255
Kwa bara la Marekani ya Kakazini kwa mpangilio huonesha hizi namba zilianza huko kisha kuja bara la Ulaya ambapo kwa nchi kama Uingereza ni +44 na Ujerumani ni +49 ambapo tunaeza kusema bara la Ulaya hizi namba zimewekwa sana sana katika kundi la makumi (10 - 99) na Marekani ni mamoja (1 - 9)
Kwa Africa namba zetu zinewekwa katika mamia (100) mfano Kenya ni +254 Tanzania +255 Somalia +253
South Africa Dialing code yao ni +27 pamoja na Egypt ni +20 ambapo ni tofauti kabisa ni nchi zingine zote za Africa.
Ningependa kujua kwanini Africa Kusini na hawa Egypt wao walipata namba zilizo katika makumi sawa na baadhi ya nchi za Ulaya na Asia?