Countdown- 1 Day to go, Zimbabwe They Decide

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,579
19,441
Keshokutwa Jumamosi tarehe 29 March 2008, wananchi wa Zimbabwe watakuwa wanapiga kura kuamu ni nani awe raisi wao kati ya Robert Mugabe, Morgan Tsvangirai na Simba Makoni.

Zimbabwe nchi ambayo imewahi kuwa nchi itoayo huduma bora za tiba barani Afrika, sasa hivi inakabiliwa na uhaba wa chakula, mfumuko mkubwa wa bei ambao umefikia asilimia 100,000.5 na idadi kubwa ya vifo ambapo umri wa wastani kwa mwanamme kufa ni miaka 37 mwanamke 34 na mtoto miaka 5.

katika wagomea hao mgombea mpya bwana Simba makoni anasema kwamba endapo kutakuwa na mauzauza katika uchaguzi huo huenda akaunganisha nguvu na bwana Tsvangirai ili kumuondoa Mugabe.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za wazimbabwe na raisi wao kiongozi wa ZNU PF na wagombea Tsvangira wa MDC na Makoni ambae ni mgombea binafsi.

0_06658600%201205325705.jpg

Mwaka 1997 Mugabe akiwa rafiki wa nchi za magharibi na Marekani akiwa na mama Hillary Clinton Ikulu ya Zimbabwe walipotembelea nchi hio, kulia ni mama Grace Mugabe.

0_18341400%201206438962.jpg

Mgombea binafsi Simba Makoni ambae aliwahi kuwa waziri wa fwedha katika serikali ya Mugabe ya ZANU-PF.

0_20092400%201206511712.jpg

Wanachama wa Movement Democratic for Change wakiwa na mabango yamunyeshao bwana Tsvangirai wiki hii. Wanadai Mugabe anatarajiwa kuvuruga uchaguzu baada ya kutawanya polisi nchi nzima katika vituo vya kupigia kura.

0_26304100%201205323461.jpg

Mugabe alifanza sherehe ya nguvu ya kuadhimisha miaka 84 ya kuzaliwa. Kushoto ni mwanae wa kike Bono na katikat anaekata keki ni mkewe Grace, mwanae wa kiume (wa kwanza) mwenye miwani Robert Jnr na mwanae wa mwisho Chatunga. Hii ilikuwa ni February 23 March mwaka huu.

0_41113200%201206463760.jpg

Kijana akiuza ndizi lakini dola milioni 5 kwa sasa ni sawa na paundi za uingereza 3 au 4.

0_45842500%201206616174.jpg

Mzee mzima Tsvangirai akihutubia wazimbabwe kwenye mkutano wa kampeni jimboni kwake Buhera tarehe 25 March 2008.

0_47376200%201206616798.jpg

Mama ana matumaini na MDC na anaipa kura za ndio.

0_48875500%201206441942.jpg

Kwenye mikutano ya ZANU-PF bado mabango ya kumuenzi Mugabe yanashikwa. Hii ilikuwa ni Jumanne wiki hii.

0_51853100%201205323170.jpg

Makoni akielezea mikakati yake katika mahojiano mjini Harare tarehe 3 mwezi March 2008.


0_95172800%201206442290.jpg

Mzee Jongwe akiondoka baada ya mkutano wa kampeni mjini Bulawayo. Hapo alisema kwamba makanisa na biashara zote ni lazima ziendeshwe na wazimbabwe weusi. Hii ilikuwa ni tarehe 23 March mwaka huu.

0_93203400%201206615991.jpg

Edgar Tekero, mmoja wa wafuasi wa karibu wa Mugabe ambae alianza kushindana nae katika chaguzi za raisi. Hapa akifanza mahojiano na waandishi wa habari tarehe 25 March 2008. Wengine waliofanza hivo ni pamoja na aliekuwa waziri wa habari Profesa Moyo ambae safari hii hajishughulishi na kutaka ukubwa.
 
Mpaka sasa hakieleweki.

Tume ya uchaguzi ambyo kama tume zingine za kiafrika ni za kuteuliwa na raisi, imekuwa ikitoa matokeo vipande vipande na mpaka pale ikifika mwisho kwamba timu ya Jongwe imekwisha-tinkering na matokea basi sijui itakuwaje.

SADC wako kimya na nchi zingine ziko kimya zikifuatilia nchi hi ama mtandaoni au kwenye luninga.

waandishi.jpg

Jamaa wa tume ya uchaguzi akitangaza matokeo nusu leo mchana, na
Rafiki yangu Sibanda ana kazi kweli hapa, kila la kheri.

Hii inanikumbusha mwaka 1995 kule Zanzibar.

Maskini bara letu la Afrika.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom