Count down: Ripoti ya Tume ya Ngwilizi...

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,987
22,515
Kumbe siko mwenyewe kwa wale wanaoshangazwa na ripoti ya Ngwilizi kucheleweshwa na kuendelea kupigwa danadana,whats going on?Je hizi kukurukakara za mbunge wa upinzani ndugu Zitto anataka kuwaaminisha magamba kwamba yeye bado ana nguvu ya kuwayumbisha mahasimu wao wakubwa CDM na hivyo wamsalie mtume?Inawezekana nikawa wrong,lakini anything is possible,ni kama vile Zitto anajitahidi kuwaonyesha wakuu wa magamba kwamba yeye bado ni relevant,na kwahiyo akituhumiwa kuhusu rushwa,basi magamba watakosa mtu wa kumtumia kukivuruga chama chake?

Tupeni ripoti ya tume ya Ngwilizi, tuwajue wabunge wala rushwa.

Taifa lilishapewa habari zenye mshtuko. Kwamba wabunge wao siyo wasafi. Ni wala rushwa wanaosahau wajibu wao wa kuwatetea wananchi. Japo waliambiwa si wote lakini ni muda sasa, tume iliundwa ila majibu yanachelewa.

Kuna wabunge walituhumiwa waziwazi. Wananchi wao wapo roho juu. Hao wanapokwenda majimboni kwao, hawapati mapokezi mazuri. Wengine tangu walipotajwa, mpaka leo hawajafika kabisa kwenye maeneo yao. Wanakwepa aibu na maswali ambayo hawana ubavu wa kuyajibu.

Maskini ya Mungu, hawana hata kipawa cha kupangua hoja inayowatuhumu kula rushwa, sasa watafanyaje? Walichobakiza ni kung'ang'ania Dar es Salaam, wakingoja majibu ya tume iliyoundwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda

Muda nao unazidi kwenda. Muda waliopewa mwanzoni ukashindwa kutoa majibu, wakaongezewa. Sasa hata kipindi walichoongezewa nacho kimepita. Tatizo lipo wapi? Au tume hiyo inayoongozwa na Brigedia Mstaafu, Hassan Ngwilizi imekwaa kisiki?

Bunge la Bajeti 2012, liliahirishwa Agosti 16, mwaka huu. Wakati wa kuahirisha, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alilitangazia bunge na Watanzania kwa jumla kuwa ameamua kuiongezea tume ya Ngwilizi wiki mbili nyingine ili iweze kukamilisha kazi yake.

Kwa mantiki hiyo, ikawa imepewa mwezi mzima, kwani siku hiyo, yaani Agosti 16, ndiyo wiki mbili za mwanzo zilikuwa zimekwisha, kwa hiyo tume ilitakiwa kuwa imekamilisha uchunguzi wake na kukabidhi ripoti kwa Spika wa Bunge ili isomwe na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Tangu Agosti 16, zimepita zaidi ya wiki tano lakini majibu ya tume hayajawekwa wazi. Suala hapa si kuingilia uhuru wa tume, ila tunahoji sababu ya ripoti kuchelewa kutolewa. Ilitakiwa uchunguzi ufanyike ndani ya wiki mbili ukamilike, sasa ni zaidi ya mwezi mmoja na wiki tatu.

Kwa mantiki hiyo, uchunguzi umechukua wiki saba. Leo tunatimiza wiki saba na siku tano, kwa hiyo bado siku mbili itimie miezi miwili. Kama imekuwa ngumu kuwanasa wenye hatia, basi tuambiwe na kama tuhuma zilikuwa za uongo, tuelezwe ili rangi ya bunge izidi kujipambanua.

Kuna mengi yapo nyuma skendo ya rushwa bungeni. Yanatakiwa kupatiwa majibu mapema kwa lengo la kukisafisha chombo hicho cha kutunga sheria. Kwa wale waliotuhumiwa kimakosa, basi wasafishwe ili kurejesha imani yao kwa wananchi wanaowaongoza.

Yapo maelezo kwamba skendo ya rushwa iliibuliwa na serikali kwa lengo la kuiwezesha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kupita. Kwamba kulikuwa na madudu mengi, kwa hiyo baadhi ya wabunge walikuwa wamejiandaa kuyaibua, jambo ambalo lingekwamisha bajeti.

Kwa mantiki hiyo, serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, ikaunda skendo hiyo ya rushwa ili kuwasulubu wabunge ambao walionekana viherehere. Kama hoja hii ina ukweli, ni wazi tuhuma kwa wabunge ni magirini. Lakini nani anajua? Tume itoe ripoti.

Ukweli utatuweka huru, hii tabia ya kupakaziana inatakiwa ikomeshwe haraka. Kuna watu wametuhumiwa mpaka kwenye mambo binafsi, kwamba wana uhusiano wa kimapenzi, kwa hiyo wanalindana. Ni wazi tuhuma zilifika kwenye kiwango kibaya mno.

Watuhumiwa wanasema tuhuma dhidi yao ni majungu, wakati wanaotuhumu, wanajiaminisha kwamba waliotuhumiwa ni wala rushwa. Utata huo utaondoka endapo ripoti yenye ukweli usiotiliwa shaka, itawekwa wazi, ikibainisha mbivu na mbichi au pumba na mchele.

Uzuri ni kwamba kila jawabu ni msala kwa upande mmoja. Endapo itaonekana wabunge walituhumiwa kula rushwa pasipo ukweli, ina maana waliozusha watakuwa na kesi ya kujibu. Bunge ni mhimili huru kabisa, kwa hiyo unaweza kuwachukulia hatua wahusika.

Kadhalika, itakapoonekana kweli wabunge wamekula rushwa, itakuwa hatua muhimu ya kukisafisha chombo hicho cha kutunga sheria za nchi kwa sababu wenye hatia itabidi watoswe. Ni wachafu, kwa hiyo lazima waondolewe ili bunge liundwe na wasafi. Tunaomba ripoti ya Ngwilizi tafadhali.

Tupeni ripoti ya tume ya Ngwilizi, tuwajue wabunge wala rushwa

Hivi karibuni Mbunge Ngwilizi alikaririwa akisema kuwa kamati yake imekamilisha ripoti yake na kwamba imeikabidhi kwa Spika wa Bunge kwa hatua zaidi.
Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya kamati hiyo zinaeleza kuwa ripoti hiyo imewatia hatiani baadhi ya wabunge waliokuwa wakituhumiwa kuhusika katika kashfa ya kuikwamisha kwa njia ya rushwa, Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Raia Mwema.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/49-uchaguzi-mkuu/26376-chadema-yambana-makinda

Ni wabunge gani hao waliotiwa hatiani?Wapi ripoti?
 
kaka hapo juu umeongea ukweli mtupu ile scandal iliibuliwa kwa makusudi bajeti ipite hakuna lolote ilikuwa umbea na mambo ambayo hayalihusu bunge moja kwa moja kama mahusiano ya wabunge wa kike na ndugu maswi, kuna waliomshtumu ZZK wameumbuka kweli baada ya kukuta wanashabikia kisichokuwepo, nawaonya mimi kama mwanasayansi ya siasa na utawala ZZK ni level nyingine nendeni pole pole kumchimba ripoti ya ngwilizi ipo hapa ninayo zaidi imemkaanga maswi na muhongo na mahawala zao wabunge wa viti maalum CCM. ndio maana nasema vijana wa ovyo wa humu JF wenye fikra za FB ongeenei kwa heshima na fanyeni tafiti msikurupuke kwa upepo.
 
kaka hapo juu umeongea ukweli mtupu ile scandal iliibuliwa kwa makusudi bajeti ipite hakuna lolote ilikuwa umbea na mambo ambayo hayalihusu bunge moja kwa moja kama mahusiano ya wabunge wa kike na ndugu maswi, kuna waliomshtumu ZZK wameumbuka kweli baada ya kukuta wanashabikia kisichokuwepo, nawaonya mimi kama mwanasayansi ya siasa na utawala ZZK ni level nyingine nendeni pole pole kumchimba ripoti ya ngwilizi ipo hapa ninayo zaidi imemkaanga maswi na muhongo na mahawala zao wabunge wa viti maalum CCM. ndio maana nasema vijana wa ovyo wa humu JF wenye fikra za FB ongeenei kwa heshima na fanyeni tafiti msikurupuke kwa upepo.
Mimi na FB wapi na wapi?weka basi hiyo ripoti badala ya maneno matupu?Maana unaongea kama Zitto mara zote kwenye michango yako.
 
tume ikiongozwa na mwanajeshi 'kama huyu brigedia' Mara nyingi matokeo yake huwa rahisi ku-predict ,maana siku zote huwa ni kusafishana!
 
Mimi na FB wapi na wapi?weka basi hiyo ripoti badala ya maneno matupu?Maana unaongea kama Zitto mara zote kwenye michango yako.
Utaisoma kaka kwa Muda muafaka na na kuhakikishia utarudi hapa kaniambia ujanja uliotumika kugeuza concentration ya Bunge badala ya kujadili bajeti wao wakajadili mambo yasiokuwepo hususan hicho kinachoitwa rushwa kumbe ni mahaba ya watu binafsi, na pia nakuuma sikio tu mama makinda hataiweka ripoti hadharani sababu inakiumbua chama chake na wabunge wao
 
Kama sio kweli kwa nini wasiiweke wazi tukajua moja? mbona inafichwa? kunani hapo? Tatizo Tanzania tumeshazoea blaa blaaa. Kila siku tume zinaundwa hakuna kinachofanyika ni upuuzi mtupu.
 
Wabunge wa cdm tunawaminia wataweka wazi kunachakuficha sikuizi mbona haya mauaji ya mwandishi wa habari asilimia kubwa watu wanaujua ukweli,
 
Utaisoma kaka kwa Muda muafaka na na kuhakikishia utarudi hapa kaniambia ujanja uliotumika kugeuza concentration ya Bunge badala ya kujadili bajeti wao wakajadili mambo yasiokuwepo hususan hicho kinachoitwa rushwa kumbe ni mahaba ya watu binafsi, na pia nakuuma sikio tu mama makinda hataiweka ripoti hadharani sababu inakiumbua chama chake na wabunge wao
Haya basi kaka,weka kopi ili tujuwe moja,ndiyo JF hii,kumkoma nyani giladi mchana kweupee!

Kwasababu hicho unachokiita muda muafaka ndiyo muda gani?Kama unaona namna gani vipi,mkabidhi Invisible copy na yeye ataibandika hapa.
 
Back
Top Bottom