Costa Awatisha Cannavaro, Sued

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 4th May 2009

Beki wa zamani wa Simba ya Dar es Salaam, Victor Costa anayechezea timu ya Agasebe De Songo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Msumbiji, amesema kiwango chake cha soka nchini humo hivi sasa kipo juu na dhamira yake ni kurudi kuchezea timu ya taifa ‘Taifa Stars’. Akizungumza kwa simu jana kutoka Msumbiji, beki huyo aliyepata kuchezea Taifa Stars, kabla ya kuumia, alisema uwezo anaouonyesha Msumbiji unamfanya ajiamini kwamba sasa anahitajika kuisaidia Taifa Stars.

“Nipo vizuri sana, sina matatizo, mguu wangu nashukuru haujanisumbua, nafanya kazi hadi jamaa wanakubali, nilijua ndio mwisho wangu wa soka baada ya kuumia, lakini Mungu amenijalia nimerudi kama mwanzo, nahitaji kuja kuisaidia Stars. “Costa uliyekuwa unamjua miaka ya nyuma, ndiyo huyo huyo amerudi sawa sawa, naamini Watanzania mashabiki wangu watafurahia taarifa ya kurejea tena kwa kiwango changu, siku si nyingi kazi yangu itaonekana huko nyumbani, ” alisema Costa.

Alisema ana imani kama Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mbrazil, Marcio Maximo atamwita katika timu, atakuwa amepata nafasi ya pekee kuweza kuonyesha uwezo wake. Kwa mujibu wa Costa kutokana na kung’ara katika timu hiyo, amepewa unahodha na yeye ni miongoni mwa wachezaji wa kutumainiwa wa timu hiyo. Costa aliumia mguu katika mazoezi ya Taifa Stars mwishoni mwa mwaka 2007 na kukaa nje ya uwanja karibu miezi saba na hata aliporejea uwanjani hakuitwa tena katika kikosi chake.

Wakati akiwa Stars, Costa alikuwa akimudu vyema namba nne, tano na sita, ambapo wakati huo beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na beki wa Mtibwa Sugar, Salum Sued hawakuwa na namba ya uhakika mbele ya beki huyo, ambapo mmoja wao ilikuwa analazimika kusubiri nje. Lakini baada ya kuumia Costa ambaye hivi sasa anajulikana kama Mohammed Costa baada ya kubadili dini, pia kuachwa katika kikosi hicho kwa beki mwingine wa kati Hamis Yusuph, Cannavaro na Sued wamekuwa ndio ‘roho’ ya Maximo Stars.

Source: HabariLeo | Costa awatisha Cannavaro, Sued
 
Naona Costa kaamua kuifuata Imani ya Baba yetu Adam na Mama wetu Hawa.
 
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 4th May 2009

Beki wa zamani wa Simba ya Dar es Salaam, Victor Costa ... Costa ambaye hivi sasa anajulikana kama Mohammed Costa baada ya kubadili dini..

Source: HabariLeo

Sasa kama tunaambiwa kabadili jina, kwa nini mwandishi wa HABARI LEO anamwita na jina la zamani?

Na sijaona hapo alipo "watisha" Cannavaro na Sued.

Hakuna medani ya vilaza Tanzania kama uandishi wa habari.
 
Back
Top Bottom