Jamani, nisaidieni ninunue dawa gani au cosmetic creams gani effective za kuondoa huu weusi wa ngozi wa kuzidi katika makwapa, magoti, elbows, and in-between the thighs? Yaani, hii inanisumbua, nipo radhi hata kupaka mgorogo. Natanguliza shukran
Hey hebu jivunie rangi yako nyeusi popote ilipo sababu ndio uafrika wako huo...Weupe ungekuwa mali, ubuyu ucngepakwa rangi..Ckushauri u2mie kemikali zozote za kukupa weupe.
ushauri wako upo, ila mimi roho inataka hivyo, ndivyo navyopenda nipo radhi kugharamika ili nifanikishe hili, sehemu hizi za mwili wangu zipo na rangi tofauti na sehemu nyinginezo, hivyo inatoa mtazamo mbaya, nataka niwe na even skin tone, and color.
, hii inanisumbua, nipo radhi hata kupaka mgorogo. Natanguliza shukran[/B][/FONT]
nataka kujaribu kwanza hizi cosmetic creams au dawa zinazopatikana over the counter (hazihitaji doctor's prescription), nione inakuwaje. huu sio ugonjwa wa ngozi ni suala la urembo kutaka ngozi pale peusi pawe rangi ya kawaida
Hapo kwenye red hapooo, kumbe rangi nyeusi si rangi ya kawaida? Na je hiyo ya kawaida ni rangi gani? Dawa ya kutakatisha madoa sugu, kwenye magoti, kwapani na sehemu hizo ulizozitaja, ni usafi tuu. kama unapooga husugui magoti yako na miguu sawia/ au kwapa lako hlioshi vizuri(au unanyoa kwa kutumia nyembe butu), hali hiyo itakutokea. Jaribu kutafuta ogeo (dodoki) laini, na unapooga hakikisha unasugua maeneo hayo kwa umakini, then kausha na paka lotion yenye hydrant ili kuzilainisha, baada ya muda utayaona mafanikio, kabla haujakimbilia hizo cream. Kuhusu mapaja well, tafuta skin tight laini il kupunguza msuguano wa ngozi. hii ni applicable kama ngozi yako ya asili ni ya weupe (brown) na kama weupe ni wa kujichubua, tafuta mkorogo tuuu.
NB: wacha kutumia mkorogo ni hatari kwa afya yako+unakushushia hadhi na thamani yako
Bhokem, mwambie huyo anafikiri mkorogo ni sifa...Kumbe ni ujinga.
jamani, wacha mtu afanye kile roho inapenda, nahitaji huo mkorogo kwa matumizi yangu na kwa vile nimeona matokeo kwa wengine (ambao husemwa kuwa wametumia mkorogo) napata imani kuwa utaweza kuondoa hilo tatizo langu. sasa basi nahitaji maelekezo tu ni wapi unapatikana (kama ni wa kununua), au labda dawa nyinginezo tafadhali
hey hebu jivunie rangi yako nyeusi popote ilipo sababu ndio uafrika wako huo...weupe ungekuwa mali, ubuyu ucngepakwa rangi..ckushauri u2mie kemikali zozote za kukupa weupe.
Aisee,Futota kwa hiyo unataka ukate pua ili uunge wajihi?Ila ukumbuke kuwa ukitaka uzuri sharti udhurike....Umejiaandaje katika hilo?Na je umeishafahamu madhara madhara yake baada ya kujichubua?
Mimi binafsi nitaendelea kukushauri kutojibadili rangi yako ya asili...Jivunie jinsi ulivyo wala ucpende kuwa km wengine sababu ndivyo ulivyoumbwa.....Nafikiri umenipata.
ungewauliza hao wengi uliowaona.