Nina upungufu wa homoni ya Testosterone, low testosterone au male hypogonadism nitapata wapi dawa ya kupaka?

Nihilist

JF-Expert Member
Jun 11, 2022
214
333
Ni muda mwingine najitokeza kuomba msaada, ushauli na mawazo kutoka kwa madaktari, wataalamu wa afya au mzoefu wa hili tatizo.

Ni baada ya kufanyiwa upasuaji (operation) ya kuondoa korodani zenye kansa na kubakia bila korodani ndipo tatizo lilipoanzia.

Nikakosa nguvu za kufanya kazi kwa muda mrefu,kupungua umakini wangu,kuwa mtu wa msongo wa mawazo kwa muda mrefu,kupoteza uwezo wa kufanya mapenzi na kupungua kwa mwili (kudhoofu mwili).

Nilirudi kumuona daktari akanieleza nina (Low testosterone (male hypogonadism) akanipatia dawa ya kuchoma kila mwezi ila inachosha, nimesikia ipo ya kupaka (gels) na vidonge (capsules).

Nimeipenda ya kupaka yaani Gel TRT au Cream,sasa je nitaipata wapi pale hospital hawa dawa hiyo msaada tafadhari....
 
Tafuta vyakula vinavyoongeza uzalishaji wa hiyo hormone uanze kula kwa wingi sana utaiboost na itaongezeka.
Kwa upande wa vyakula najitahidi mno mlo kamili lakini bado sipo sawa
 
Sasa vyakula bila engine ya kuzalisha hormone inakuaje...... Naona jamaa anahitaji hormone direct ila sio vitu vya kusaidia kuzalisha hormone maana mitambo si haipo ya uzalishaji
Asante kwa kunielewa
 
Kwaiyo hapo kuhusu kuzalisha shahawa haipo no kutia mimba anyaway pole sana, ni kama umehasiwa tafuta ya vidonge ukisema ul vyakula haitosaidia utaishia kunenepa tu
Naomba kama unaifahamu yeyote inayopatikana kwa urahisi pharmacy unisaidie jina tafadhari
 
Hapa kwa msaada wa haraka na umakini inabidi uende kwa daktari kabisa au kama hauna uwezo nenda pharmacy yenye wataalamu.. hapa utapewa majibu ila sio sahihi kwenda kununua hiyo dawa moja kwa moja
Nitajihidi kuendelea kufuatilia kwa madaktari wengine, licha ya kupata dawa ya kuchoma sindano tu kutoka kwao ila naamini hapa wapo madaktari wazuri na wakubwa wanaoweza nishauri pia...
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom