mkolaj
JF-Expert Member
- Mar 24, 2014
- 3,023
- 1,092
Hukumu ya Mart Nooij na Taifa Stars kuanza leo;
Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" leo usiku itatupa karata yake ya kwanza dhidi ya Swaziland katika michezo ya mashindano ya COSAFA.
Taifa Stars inashiriki michuano hio kama timu mwalikwa ikiwa imepangwa kundi B pamoja na timu za mataifa ya Lesotho, Swaziland na Madagascar.
Stars inahitaji ushindi katika mechi ya leo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuibuka kinara wa kundi B na kupata tiketi ya kucheza robo fainali dhidi ya Ghana.
Mechi ya mwisho baina ya Taifa Stars na Swaziland ilimalizika kwa suluhu ya mabao 1-1. Bao la Taifa Stars lilifungwa na Thomas Ulimwengu ambae leo hatakuwepo katika mchezo huo.
Pambano la leo litachezwa kwenye uwanja wa Royal Bafokeng, likitarajiwa kuanza saa 2:30 kwa saa za Afrika Mashariki.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
Kila la kheir Taifa Stars.
===================
===================
Matokeo ya Mwisho: Swaziland 1 - 0 Tanzania