Corruption can blind People, Rushwa ya Lowassa ni zaidi ya Tindikali

Weston Songoro

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2014
Posts
2,793
Reaction score
1,086
Wanabodi, sote tunafahamu kuwa tindikali ni kemikali mbaya sana ambayo hakika mtu akimwagiwa usoni ni nadra mtu huyo kuendelea kuona.

Wengi waliopatwa na madhara ya kumwagiwa tindikali hakika wamebaki kuwa vilema na wengi wao wakiwa ni vilema wa kutoona, upofu.

Wapo wachache ambao hubahatika kuona wakimwagiwa tindikali lakini maisha yao yanaendelea kuwa ya taabu na mara kwa mara wanatakiwa kuwa chini ya uangalizi wa matabibu.

Si lengo langu kuelezea athari za tindikali halisi kwa maisha ya binadamu. Tindikali mbaya zaidi ni hii ya Rushwa ambayo Watanzania wengi tumemwagiwa na hivyo wengi wetu tumebaki kuwa vilema. Rushwa imetupofusha watu. Rushwa imetufanya tushindwe kutenganisha jema na baya.

Rushwa imebadili hali ya mtu. Yule aliye mbaya leo hii anakumbatiwa na kupambwa kwa mapambio ya kila aina. Rushwa. Rushwa. Rushwa.

Na rushwa iliyotokana na ufisadi ni mbaya sana kwa vile husambaa kwa kasi ya ebola ambapo athari zake huwapata hata wale wa mbali.

Ni hivi karibuni tumeshuhudia mtu ambaye anajulikana kuwa ni fisadi akipambwa majukwaani ambapo rushwa imewafanya watu hao wamuone Edward Lowasa kama lulu ama malaika aliyeteremshwa kutoka mbinguni kuja kuwasaidia Watanzania.

Baadhi ya vijana kadhaa wamejikusanya pamoja na kuunda makundi kadhaa kwenye mitandao na kujiita Team Lowasa.

Hawa vijana wanafahamu kuwa jina Lowasa ni jina baya kutokana na ufisadi wa Edward Lowasa ila kwa vile rushwa imetamalaki, leo hii jina hilo badala ya kuwa baya, limegeuka kuwa jina zuri na watu wengi wametamani kujinasibisha nalo. Rushwa.

Akina mama ni watu makini sana inapofika kwenye masuala ya kufanya maamuzi. Lowasa alilitambua hilo. Hivyo, ili kuwavuruga na wasifanye maamuzi kutokana na utashi wao, kawatia upofu kutokana na rushwa pale alipojipenyeza ndani yao na kujifanya mtu wa kusaidia vikundi mbalimbali. Rushwa.

Viongozi wa kiroho tunawategemea kurekebisha pale ambapo jamii inakuwa imeharibiwa na wanasiasa. Dini inakuwa kimbilio kwa waliokata tamaa. Ila kutokana na rushwa, viongozi wa kiroho kwa sasa wamegeuka kuwa wapambe wa wanasiasa na fedha za ufisadi zinatumika kujenga nyumba za ibada na kuwasaidia viongozi wa kidini. Leo hii rushwa imewafanya viongozo hao wa kiroho wawe vipofu. Mtu kama Mchungaji Gwajima amefikia hata kusema kuwa wale wasiompenda Lowasa wale malimao. Hakika Rushwa ni mbaya sana.

Katika wanasiasa ambao nilikuwa nawaheshimu basi Kingunge Ngombale Mwiru ni mmojawapo. Ni mtu aliyekuwa na maono kabla hajapofuliwa na rushwa. Kingunge wa leo si yule wa enzi za Mwalimu. Laiti kama baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere angefufuka leo na kushuhudia jinsi Kingunge anavyosimama majukwaani na kumpamba Lowasa angeshangaa sana. Rushwa imemfanya Kingunge asione ubaya wa Lowasa. Zipo taarifa kwamba Kingunge kapata zaidi ya milioni 300 na Lowasa kufanya tu kazi ya kumsafisha majukwaani. Rushwa.

Upo usemi usemao kuwa ya Kaisari mpe Kaisari na ya Mungu mpe Mungu. Leo hii rushwa imefanya watu wapofuke. Leo hii mtu kama Madabida anasimama jukwaani na kumfananisha Mtume Muhammad na Lowasa na watu wanashangilia. Rushwa. Rushwa. Rushwa. Hivi ni kweli Madabida hajui kuwa dini yake inasema kuwa Mtume Muhammad ni kiigizo chema hivyo kumfananisha na Lowasa ambaye ni fisadi papa ni kumdhalilisha Mtume wa Mwenyezi Mungu? Nina hakika Madabida anafahamu hilo ila kwa vile rushwa imempofusha, ameamua kutoa statement ambayo nina hakika inalaaniwa na wenye dini yao. Haya matamko yanayoanza kutolewa na viongozi wa dini ya kiislam ni ishara kuwa madabida kalikoroga.

Ninavyojua mimi ni kwamba mtu unapochaguliwa ama kuteuliwa kushika nafasi fulani unapaswa kuwa mwadilifu na utende haki bila kubagua. Viongozi wa CCM wa mikoa ndio walezi na wasimamizi wa chama ngazi ya mikoa. Ila kutokana na rushwa na ufisadi, leo hii baadhi ya wenyeviti wa mikoa ambao kwa nyadhifa zao wanashiriki vikao vya maamuzi ndani ya chama wameamua kujinasibisha kwa Edward Lowasa. Hawa viongozi wa sasa wamekuwa vipofu na wamekuwa wakiacha maeneo yao ya kazi na kufuatana na Edward Lowasa. Rushwa na ufisadi umewapofusha.

Hakika mifano ipo mingi sana na nina hakika hata member wenzetu humu nao wamepofushwa na rushwa na ufisadi wa Edward Lowasa. Ila nawaomba msikate tamaa. Lipo tumaini jipya linakuja na hakika wale wote waliopofushwa na rushwa na ufisadi wa Lowasa wataona aibu. CCM haitafanya kosa. Itatuletea mtu ambaye anaakisi mambo yanayopendwa na Watanzania wengi na si huyu fisadi Lowasa ambaye amewafanya baadhi ya watu wawe vipofu.
 
Tanzania bila ya rushwa inawezekana. Akina Madabida, Msukuma, Kingunge na wengineo mtaficha wapi sura zenu baada ya fisadi Lowasa kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha Urais?
 
Nakubaliana na wewe Chabruma. Chama kinapaswa kuchukua hatua dhidi ya hawa wenyeviti ambao wanakiuka miikomya uongozi. Ni wakati sasa wa chama kufanya kile ambacho wananchi wanakitaraji
 
Vijana wote wangekuwa kama wewe Taifa hili lingefika mbali sana leo Mtume wa Mwenyezi Mungu anafananishwa na Lowassa? RUSHWA HATARI SANA.
 
Sasa inatosha. Mwisho wa Rushwa ni sasa
 
Hata sisi Wakristo tunaamini kuwa PESA ndiyo iliyopelekea Yesu kusulubiwa. MADABIDA ni sawa na YUDA ESKARIOTI.
 
Nakubaliana na wewe Chabruma. Chama kinapaswa kuchukua hatua dhidi ya hawa wenyeviti ambao wanakiuka miikomya uongozi. Ni wakati sasa wa chama kufanya kile ambacho wananchi wanakitaraji
Lowassa karibia ataitwa Mume wao, kwa jinsi alivyowqpumbaza kwa rushwa anaweza hata kuwafanya wake.
 
Tanzania bila ya rushwa inawezekana. Akina Madabida, Msukuma, Kingunge na wengineo mtaficha wapi sura zenu baada ya fisadi Lowasa kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha Urais?
Mkuu, mla rushwa hana tofauti na Kahaba anayejiuza, wote hao huwa hawana mshipa wa aibu.
 
Wanabodi, sote tunafahamu kuwa tindikali ni kemikali mbaya sana ambayo hakika mtu akimwagiwa usoni ni nadra mtu huyo kuendelea kuona.

Wengi waliopatwa na madhara ya kumwagiwa tindikali hakika wamebaki kuwa vilema na wengi wao wakiwa ni vilema wa kutoona, upofu.

Wapo wachache ambao hubahatika kuona wakimwagiwa tindikali lakini maisha yao yanaendelea kuwa ya taabu na mara kwa mara wanatakiwa kuwa chini ya uangalizi wa matabibu.

Si lengo langu kuelezea athari za tindikali halisi kwa maisha ya binadamu. Tindikali mbaya zaidi ni hii ya Rushwa ambayo Watanzania wengi tumemwagiwa na hivyo wengi wetu tumebaki kuwa vilema. Rushwa imetupofusha watu. Rushwa imetufanya tushindwe kutenganisha jema na baya.

Rushwa imebadili hali ya mtu. Yule aliye mbaya leo hii anakumbatiwa na kupambwa kwa mapambio ya kila aina. Rushwa. Rushwa. Rushwa.

Na rushwa iliyotokana na ufisadi ni mbaya sana kwa vile husambaa kwa kasi ya ebola ambapo athari zake huwapata hata wale wa mbali.

Ni hivi karibuni tumeshuhudia mtu ambaye anajulikana kuwa ni fisadi akipambwa majukwaani ambapo rushwa imewafanya watu hao wamuone Edward Lowasa kama lulu ama malaika aliyeteremshwa kutoka mbinguni kuja kuwasaidia Watanzania.

Baadhi ya vijana kadhaa wamejikusanya pamoja na kuunda makundi kadhaa kwenye mitandao na kujiita Team Lowasa.

Hawa vijana wanafahamu kuwa jina Lowasa ni jina baya kutokana na ufisadi wa Edward Lowasa ila kwa vile rushwa imetamalaki, leo hii jina hilo badala ya kuwa baya, limegeuka kuwa jina zuri na watu wengi wametamani kujinasibisha nalo. Rushwa.

Akina mama ni watu makini sana inapofika kwenye masuala ya kufanya maamuzi. Lowasa alilitambua hilo. Hivyo, ili kuwavuruga na wasifanye maamuzi kutokana na utashi wao, kawatia upofu kutokana na rushwa pale alipojipenyeza ndani yao na kujifanya mtu wa kusaidia vikundi mbalimbali. Rushwa.

Viongozi wa kiroho tunawategemea kurekebisha pale ambapo jamii inakuwa imeharibiwa na wanasiasa. Dini inakuwa kimbilio kwa waliokata tamaa. Ila kutokana na rushwa, viongozi wa kiroho kwa sasa wamegeuka kuwa wapambe wa wanasiasa na fedha za ufisadi zinatumika kujenga nyumba za ibada na kuwasaidia viongozi wa kidini. Leo hii rushwa imewafanya viongozo hao wa kiroho wawe vipofu. Mtu kama Mchungaji Gwajima amefikia hata kusema kuwa wale wasiompenda Lowasa wale malimao. Hakika Rushwa ni mbaya sana.

Katika wanasiasa ambao nilikuwa nawaheshimu basi Kingunge Ngombale Mwiru ni mmojawapo. Ni mtu aliyekuwa na maono kabla hajapofuliwa na rushwa. Kingunge wa leo si yule wa enzi za Mwalimu. Laiti kama baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere angefufuka leo na kushuhudia jinsi Kingunge anavyosimama majukwaani na kumpamba Lowasa angeshangaa sana. Rushwa imemfanya Kingunge asione ubaya wa Lowasa. Zipo taarifa kwamba Kingunge kapata zaidi ya milioni 300 na Lowasa kufanya tu kazi ya kumsafisha majukwaani. Rushwa.

Upo usemi usemao kuwa ya Kaisari mpe Kaisari na ya Mungu mpe Mungu. Leo hii rushwa imefanya watu wapofuke. Leo hii mtu kama Madabida anasimama jukwaani na kumfananisha Mtume Muhammad na Lowasa na watu wanashangilia. Rushwa. Rushwa. Rushwa. Hivi ni kweli Madabida hajui kuwa dini yake inasema kuwa Mtume Muhammad ni kiigizo chema hivyo kumfananisha na Lowasa ambaye ni fisadi papa ni kumdhalilisha Mtume wa Mwenyezi Mungu? Nina hakika Madabida anafahamu hilo ila kwa vile rushwa imempofusha, ameamua kutoa statement ambayo nina hakika inalaaniwa na wenye dini yao. Haya matamko yanayoanza kutolewa na viongozi wa dini ya kiislam ni ishara kuwa madabida kalikoroga.

Ninavyojua mimi ni kwamba mtu unapochaguliwa ama kuteuliwa kushika nafasi fulani unapaswa kuwa mwadilifu na utende haki bila kubagua. Viongozi wa CCM wa mikoa ndio walezi na wasimamizi wa chama ngazi ya mikoa. Ila kutokana na rushwa na ufisadi, leo hii baadhi ya wenyeviti wa mikoa ambao kwa nyadhifa zao wanashiriki vikao vya maamuzi ndani ya chama wameamua kujinasibisha kwa Edward Lowasa. Hawa viongozi wa sasa wamekuwa vipofu na wamekuwa wakiacha maeneo yao ya kazi na kufuatana na Edward Lowasa. Rushwa na ufisadi umewapofusha.

Hakika mifano ipo mingi sana na nina hakika hata member wenzetu humu nao wamepofushwa na rushwa na ufisadi wa Edward Lowasa. Ila nawaomba msikate tamaa. Lipo tumaini jipya linakuja na hakika wale wote waliopofushwa na rushwa na ufisadi wa Lowasa wataona aibu. CCM haitafanya kosa. Itatuletea mtu ambaye anaakisi mambo yanayopendwa na Watanzania wengi na si huyu fisadi Lowasa ambaye amewafanya baadhi ya watu wawe vipofu.

RUSHWA na UFISADI ni kansa inayo iua ccm taratiiiibu na kudhihirisha kuwa rushwa imetamalaki ndani ya Chama chetu si tuaona pamoja na viashiria lukuki vya kuwepo na rushwa kwa watangaza nia wengi wa ccm TAKUKURU iko kimya kana kwamba haipo vile.
 
Back
Top Bottom