Mabibi na mabwana hali inaendelea kuwa si hali. Sisi tulio hatarini sauti zetu lazima zisikike. Kwa mwelekeo uliopo ndiyo tumeshatolewa kafara hivyo.
Jana tumemzika kigogo wa BOT (Joachim Sayi Nsunga) RIP, huko Dutwa Bariadi, Simiyu. Huyu bwana alikuwa mhasibu mkuu BOT makao makuu, Dodoma.
Amefariki juzi pale Benjamin Mkapa. Hakuwa mtu mdogo kwani angalau aliweza kutumia ventilator.
Pana mwelekeo kabambe wa kudhibiti taarifa za vifo. Kuzifanya taarifa za vifo vya vigogo kuwa ni nyara za serikali.
Wazee na wenye magonjwa mengine, sisi pia kama walipa kodi ni muhimu sana tukapaza sauti zetu vilivyo. Hatustahili kutelekezewa janga. Tunayo haki ya kuishi kama ilivyo kwa watu wengine.
Sisi tunalipa kodi na wengine wetu tumelipa sana kodi labda kuliko hata hawa ambao leo wanawashwa sana na pilipili wasizo zila kutusemea sisi.
Propaganda za vijiweni kuwa ugonjwa huu hauuwi ila hofu. Ugonjwa huu tiba yake ni mazoezi. Ugonjwa huu tiba yake ni lishe, malimao na tangawizi. Ugonjwa huu tiba yake ni nyungu n.k.
Yote hayo tokea vijiweni hayatusaidii sisi tulio wahanga zaidi.
Wito kwa serikali:
"Sisi tulio wahanga wa kesho wa ugonjwa huu tunaidai haki yetu ya kuishi. Tunawaona wenzetu wanavyopukutika. Kama mnatu 'kana' tukiwa hai, nasi tuta 'wakana' ninyi tukiwa hai."
Tafadhalini sana waachieni wataalamu wa afya kushika hatamu za uongozi wa vita dhidi ya ugonjwa huu. Kwanini ombi hili ni kubwa mno kwenu?
Hadi tufe wangapi?
Kwanini nyie msiokuwa katika hatari ya ugonjwa huu mmekuwa sana wa kutusemea, hali kufa twafa sisi?
Mara ooh mliona wapi mwana michezo kafa kwa Corona? Jibu ni kuwa hatujui. Kwani hazipo takwimu hizo kama ambavyo hatujui pia kama kuna machangudoa wowote wamekufa kwa Corona.
Hivyo pia hatuwezi kusema kuwa uchangudoa ni kinga ya Corona.
Hivi ni wapi palipo na wana michezo wazee au wenye magonjwa mengine? Mbona kuchezana shere hivi?
Hebu tusitoane kafara mchana kweupe namna hii.
Ninawasilisha.