Corona; sekta ya utalii kudorora, sekta ya kilimo, vyakula na biashara mitandaoni kuchanua. Tujipange kama nchi

Conwel Ngani

Senior Member
Sep 16, 2018
134
149
Salam

Kutokana na janga la corona itachukua miaka mingi sana kurudisha miingiliano tuliyokuwa nayo hapa duniani kama dawa ya corona haitapatikana na njia za upimaji hazitaboreshwa. Corona italeta mfumo mpya kabisa wa maisha, kusafiri baina ya nchi na nchi kutapungua kwa kiwango kikubwa sana la sivyo ukubali kupoteza siku 28 za kujitenga (quarantine). Hapa namaanisha ukienda Kenya kule utajitenga kwa siku 14 na ukirudi Tanzania utajitenga tena kwa siku 14 labda kama hii kitu kukaa quarantine itaondolewa.

Kwa kuwa Mungu kaijalia nchi yetu ardhi kubwa na vyanzo vya maji vya kutosha ni wakati muafaka kuwekeza zaidi kwenye kilimo cha kisasa na viwanda vya bidhaa za vyakula ili kuinua uchumi wetu kwasababu utalii unaweza kudora kwa muda mrefu sana. Pia ukizingatia nchi kama DRC, Kenya, Burundi, Rwanda, Uganda na Sudani hututegemea sana kwa upatikanaji wa chakula. Na kwa kuwa Uganda, Kenya na Rwanda wako lockdown basi demand ya bidhaa za vyakula itaongezeka sana.

Pia ni wakati sahihi kwa serikali kuboresha sera za biashara mitandaoni na kutoa elimu kuhusiana na hili na wafanyabiashara kuwekeza katika hili ili kuruhusu kuuza, kununua na kufanya malipo kwa njia ya mtandao ili kupunguza miingiliano pamoja na kuziba pengo la kutokusafiri nje ya nchi.

Pia katika kuboresha biashara za mitandaoni binafsi nahisi shirika letu la Posta linatakiwa kufanyiwa mageuzi makubwa sana ili kukidhi hitaji hili.

Kwa kuwa kuna maisha baada ya corona ni vyema tukaanza kujipanga katika hili.
 
  1. Tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara
  2. Kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi
 
Bandiko Bora kabisa hili. Watu waingie shambanj jamani
Salam

Kutokana na janga la corona itachukua miaka mingi sana kurudisha miingiliano tuliyokuwa nayo hapa duniani kama dawa ya corona haitapatikana na njia za upimaji hazitaboreshwa. Corona italeta mfumo mpya kabisa wa maisha, kusafiri baina ya nchi na nchi kutapungua kwa kiwango kikubwa sana la sivyo ukubali kupoteza siku 28 za kujitenga (quarantine). Hapa namaanisha ukienda Kenya kule utajitenga kwa siku 14 na ukirudi Tanzania utajitenga tena kwa siku 14 labda kama hii kitu kukaa quarantine itaondolewa.

Kwa kuwa Mungu kaijalia nchi yetu ardhi kubwa na vyanzo vya maji vya kutosha ni wakati muafaka kuwekeza zaidi kwenye kilimo cha kisasa na viwanda vya bidhaa za vyakula ili kuinua uchumi wetu kwasababu utalii unaweza kudora kwa muda mrefu sana. Pia ukizingatia nchi kama DRC, Kenya, Burundi, Rwanda, Uganda na Sudani hututegemea sana kwa upatikanaji wa chakula. Na kwa kuwa Uganda, Kenya na Rwanda wako lockdown basi demand ya bidhaa za vyakula itaongezeka sana.

Pia ni wakati sahihi kwa serikali kuboresha sera za biashara mitandaoni na kutoa elimu kuhusiana na hili na wafanyabiashara kuwekeza katika hili ili kuruhusu kuuza, kununua na kufanya malipo kwa njia ya mtandao ili kupunguza miingiliano pamoja na kuziba pengo la kutokusafiri nje ya nchi.

Pia katika kuboresha biashara za mitandaoni binafsi nahisi shirika letu la Posta linatakiwa kufanyiwa mageuzi makubwa sana ili kukidhi hitaji hili.

Kwa kuwa kuna maisha baada ya corona ni vyema tukaanza kujipanga katika hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom