Corona kusababisha kafara la nchi?

Nov 21, 2018
29
26
Dunia kwa sasa imepigwa na bumbuazi kutokana na virus wanaoitwa Corona. Wapo wanaodai huenda vikawa ni mambo ya kuharibiana kibiashara kwa kuamini ya kwamba huenda ikawa Corona ilitengenezwa na Wamarekani ili kuchafua biashara ya China na wapo wanaoamini ya kwamba ni miongoni mwa mapigo ya Mungu tu kwa watu wake.

Twende kwenye pointi husika ya kafara la nchi. Siku chache zilizopita kumetokea na wenzetu waliopo China kuomba Serikali iwarudishe nyumbani.

Hali kadhalika kiuhalisia hata ndugu zao wanatamani kuona watoto wao wanarudi nyumbani na kwa sasa inavyosemekana China imefunga mipaka yake kwa maana hakuna watu kusafiri kwenda au kuingia kwa baadhi ya sehemu.

Sasa hao ndugu zetu watarudi vipi? Na je serikali itachukua hatua gani kwa hao watu kwa maana nchi kama China kushindwa kupambana na Corona mpaka kufikia watu zaidi ya 1000 kufa ni dhahiri shahiri ya kwamba ukifika Tanzania ni zaidi ya watu waliokufa china itatokea kutokana na miundombinu ya nchi yetu kuwa mibovu na undugu wa kushikana shikana. Yote hayo tumwombe Mungu aepushie mbali.

Kuhusu hao ndugu zetu watarudi? Je, tuna chombo cha kupima afya zao? Je, tuna chombo cha kufuatilia afya zao? Nionavyo mimi hawa watatolewa kafara la nchi kukomboa wengine dhidi ya Corona.

Kiukweli inauma na itaendelea kuuma kuona mwanao yuko anaomba msaada wa mzazi kumsaidia lakini anashindwa kutokana na taratibu za nchi.

Je, wandugu serikali ifanye nini juu ya hao wenzetu?
 
Nadhani serikali inatakiwa kuhakikisha inagharamia mahitaji yao yote kwa ukaribu zaidi wakiwa huko walipo sasahivi, na kama pameonekana ni mahali salama wao waachwe tu huko huko maana ikitokea wamekuja nchini wakiwa wameathiriwa na virusi itakua hatari zaidi.

Nchi bado inapambana na malaria akiingia huyo corona tutakufa kwa mafungu
 
Nashauri warudishwe ila watengwe katika kisiwa kimoja ambacho hakikaliwi na watu huko ukara kwa muda wa angalau siku 21.
 
Dooh kama ushaangalia sana movie zinazohusu ZOMBIE haya ndio yanaelezewaga sana kwenye storylines ya movie hizo, malanyingi sehemu ikiwa imepata athari ya mazombi inatengwa na kudhibitiwa zombie wasiingie sehemu zisizoathilika Ishu unakuja endapo muathilika mmoja tu ataingia kwenye sehemu salama bana basi wote mumeathilika hapo...angalia Movie ya 28 Days Later jamaa kaenda kumchukua mkewe kisa anampenda kumbe kaathilika kosa hilo lilifanya mji mzima uathilike, Day Of The Dead walimchukua Zombie mmoja tu akaja kuathili Base mzima.

Kutokona na lesson nilipopata kwenye hizo movie nasema hao jamaa waachwe tu hukohuko.

Portfolio | 2020
 
Back
Top Bottom