kyarluta
Member
- Oct 28, 2019
- 24
- 12
Leo nimeongea na rafiki yangu ambaye ni daktari. Yuko wilaya ya Bukombe na anamiliki hospitali. Katika kipindi chote cha Corona, hospitali yake haijawahi kupokea mgonjwa mwenye viashiria vya korona. Kule kwa korona haipo.
Ametoa ushuhuda kwamba, utaratibu wa kunawa mikono Mara kwa mara, umepunguza magonjwa. Amenitajia magonjwa kama Kuhara, kipindupindu na magonjwa ya macho.
Anasema kuwa hata mapato yake yamepungua kutokana na wagonjwa wa aina hiyo kupungua.
Huu ni ushindi mkubwa kwa walio wengi. Kinachotakiwa ni kutolegeza juhudi hii ya usafi wa mikono wa mara kwa mara. Hakuna asiyejua kwamba gharama za matibabu ziko juu. Magonjwa yanapunguza uchumi wa familia. Tukishinda magonjwa haya itabakia issue moja ambayo haiepukiki nayo ni kuhudumia wajawazito.