Mabibi na mabwana kwa hakika hekima ni uhuru.
Bila ya kupepesa macho, inataarifiwa kuwa pale UDSM wamechukua hatua hii ya msingi sana:
Japo pale #5 mwishoni mwishoni pana ka ukakasi, ni hatua kama hizi tunazoihitaji pia serikali kuzichukua. Hasa hasa kudhibiti mikusanyiko ya watu na kuwahami wale walio kwenye hatari zaidi.
Hayo yapo mikononi mwa serikali na mwenye dhamana nayo ni wao.
UDSM wameonyesha njia. Wenye macho hawaambiwi tazama.
Serikali nanyi fanyeni kama hayo muone kama hatutawapongeza kwa bashasha. Zaidi sana kabidhini jukumu la vita hivi dhidi ya ugonjwa huu kwa wataalamu wetu wa afya. Kwa hakika watatuvusha.
Ni hatua njema kukiainisha ki usahihi chuo hiki kutoka katika dhana ya jalala inayoendelea kumea kwa kutokukemea yaliyo ndivyo sivyo.
Hilo likikihusu chuo hiki kikongwe moja kwa moja na ma alumni wake wote popote kule waliko.
Nani ajuaye kama uthubutu wa wana Dar es salaama kwenye kujitambua una mchango gani kwenye hili?
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. La UDSM tumelisikia, tunawasubiria na wengine wote wenye kufanana nao. Hasa hasa tunaisubiria serikali kufanya sehemu yake.
Kila dakika inayopita bila ya kuchukua hatua ni dakika iliyopotea kwenye jitihada za kuokoa maisha.
Ninawasilisha.

Corona: Dar es Salaam Wananchi wafanya kweli. Hongereni sana
Mabibi na Mabwana hapa ni Dar katika mapambano dhidi ya Corona. Kwa hakika hawa wameonyesha njia kwani hizi ni jitihada binafsi baada ya kutambua ugonjwa huu upo na biashara ni asubuhi. Kama vifaranga vya kuku vile kwa hakika hawa wana chakura kivyao kivyao: Wa mikoa mingine zingatieni...
www.jamiiforums.com