CONSPIRACY OVER THE COUNTRY

Chukawe Jr

New Member
Nov 20, 2016
2
20
Ndugu zangu watanzania kuna mpango mkubwa unaendelea ambao hauna nia njema na nchi yetu. Mpango huo umeitwa kwa jina la "Greater Again" na una malengo ya kuhakikisha mfumo dhalimu wa Kiliberali unarudi katika nafasi yake Nchini.

Mfumo huu ndio chungu ya kuporomoka kwa maadili ya viongozi wa UMMA pamoja na kuongezeka kwa Ufisadi na Wizi wa Mali za umma. Kama ilivyo mifumo mingine, mfumo huu umeundwa na watu wa nyanja mbalimbali wakiwemo wafanya biashara, baadhi ya wanasiasa, wasanii wa Bongo flava nk.

Wakiongozwa na kauli mbiu inayosema "STRONGER TOGETHER" baadhi ya wafanyabiashara wameamua kuwaunganisha waliokosana kutokana na kutokuelewana katika uchaguzi wa mwaka 2015 hali iliyosababisha mtikisiko mkubwa katika ngome ya uliberali Nchini.

Kauli mbiu hii wameamua kuitumia ili kuliunganisha kundi hilo kubwa Nchini na lenye nguvu ya Mali na Fedha ili kujiunganisha upya "GREATER AGAIN " na kuchukua Nchi yao ambayo walijipanga kuichukua Toka SIASA ZA UJAMAA NA KUJITEGEMEA na kufanikiwa miaka ya 1990.

Hata wao wamekubali kuwa kutofautiana kwao kuliwafanya wavurugike na kukosa nguvu katika kuitetea jumuiya hiyo ya Kiliberali kutokana tu na mgongano wa maslahi binafsi. Jambo hilo linafanywa katika usiri mkubwa sana.

Katika mpango huo wamejipanga kuwashawishi viongozi hao ili kumaliza tofauti zao na kuliunda kundi mpya kwa nguvu kubwa. Katika mpango huu ulioitwa GREATER AGAIN umegawanyika katika phase na phase ya kwanza ni Kufanya MARIDHIANO kwa maasimu 2 katika siasa. Phase hii inaitwa kwa jina la RE-ESTABLISHMENT.

Ushawishi unaotumika ni kuwakutanisha na kusuluhisha tofauti yao kwa kuwapa mkakati wa kuhakikisha watoto wao wanachukua URAIS 2025. Maandaliz hayo yameshaanza kufanyika namna ya kumfanya mtoto wa R1 kuchukua form na mtoto wa R2 kuwa waziri Mkuu.

Mtoto wa R2 kwa mara ya kwanza atagombea ubunge jimbo la Monduli ili akidhi vigezo vya kuwa waziri Mkuu kwani katiba inatamka dhahiri kuwa ili uwe waziri Mkuu lazima uwe Mbunge wa KUCHAGULIWA.

Aidha imeandaliwa kuwa R1 au R2 itaamuliwa agombee upande upi Kulingana na hali itakavyokuwa.

Mpango huu umekuja baada ya kuona msimamo wa Mh. Rais Magufuli hauko upande wao hivyo wakaamua kujipanga ili Chama kisije leta Mtu mwenye mlengo wa kijamaa na itikadi za mwalimu na misimamo kama ya Rais Magufuli.

Kundi hili ndio hao waliokuwa wakipitisha mizigo bila kulipia kodi, ndio hao waliokuwa wakiruhusu mizigo itoke bandarini bila kulipiwa Kodi, Kuuwa tembo na kusafirisha twiga hai, Waingizaji na wauzaji wa madawa ya kulevya, waliojihusisha na Wizi wa MABILION YA SHILINGI katika Serikali YETU, ndio hao waliouwa shirika la ndege ATC na Shirika la Reli nchini nk.

Ikumbukwe maendeleo yoyote yanayoletwa na serikali hatuna budi kuyalinda. Hivyo kutokana na kuwepo kwa mpango huu nashauri yafuatayo

1) Viongozi wa Chama wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama wajiandae mapema kuwakabili ili kunusuru mpasuko wa kisiasa zaidi ya ule wa 2015.

2 ) Mipango ya namna hii isipewe nafasi hata kidogo kwa kuhakikisha tunaianika na kuikemea mapema

3 ) Viongozi wa chama wasiyumbishwe kwa ajili ya kutaka kuendelea baada ya awamu ya 5 na kukubali kununulika ili kufanikisha mipango ya namna hii.

4 ) Tusijisahau

5 ) Lazima wanachama tushikamane ili kupambana na nia Ovu za namna hii ndani ya CHAMA CHETU.

6) Kauli ya LOWASA kwamba marafik zake waliobaki CCM waendelee kushirikiana tusiiipuuze hata kidogo.

Tutaendelea kuhabarishana Kitakachokuwa kinajili katika mpango huu mchafu hasa kwa Phase inayoendelea.

VIVA MAGUFULI VIVA CHAMA CHA MAPINDUZI

NA
CHIKAWE JR.
 
silasc

JF-Expert Member
Feb 10, 2013
3,356
2,000
Ungekuwa objective ktk uandishi wako, hii mada ingekuwa msaada sana. Lakini umeshindwa hata kuwataja wahusika kwa majina na hata vikao wanavyokaa kupanga hayo mambo vinafanyikia wapi.
Umeandika kisiasa zaidi na si ktk dhamira ya kuwafichua hao wadhalimu.
 
IGWE

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
9,206
2,000
Ndio maana ya siasa...sijaona baya lolote hapo.
.....mwambie mkuu wa kaya awe anasikiliza na wenzake(ushauri) ndio itakuwa pona yenu.
....say say-Karma has no menu,you get served what you deserve.
 
JFK wabongo

JF-Expert Member
Aug 11, 2015
3,755
2,000
Ndugu zangu watanzania kuna mpango mkubwa unaendelea ambao hauna nia njema na nchi yetu. Mpango huo umeitwa kwa jina la "Greater Again" na una malengo ya kuhakikisha mfumo dhalimu wa Kiliberali unarudi katika nafasi yake Nchini.

Mfumo huu ndio chungu ya kuporomoka kwa maadili ya viongozi wa UMMA pamoja na kuongezeka kwa Ufisadi na Wizi wa Mali za umma. Kama ilivyo mifumo mingine, mfumo huu umeundwa na watu wa nyanja mbalimbali wakiwemo wafanya biashara, baadhi ya wanasiasa, wasanii wa Bongo flava nk.

Wakiongozwa na kauli mbiu inayosema "STRONGER TOGETHER" baadhi ya wafanyabiashara wameamua kuwaunganisha waliokosana kutokana na kutokuelewana katika uchaguzi wa mwaka 2015 hali iliyosababisha mtikisiko mkubwa katika ngome ya uliberali Nchini.

Kauli mbiu hii wameamua kuitumia ili kuliunganisha kundi hilo kubwa Nchini na lenye nguvu ya Mali na Fedha ili kujiunganisha upya "GREATER AGAIN " na kuchukua Nchi yao ambayo walijipanga kuichukua Toka SIASA ZA UJAMAA NA KUJITEGEMEA na kufanikiwa miaka ya 1990.

Hata wao wamekubali kuwa kutofautiana kwao kuliwafanya wavurugike na kukosa nguvu katika kuitetea jumuiya hiyo ya Kiliberali kutokana tu na mgongano wa maslahi binafsi. Jambo hilo linafanywa katika usiri mkubwa sana.

Katika mpango huo wamejipanga kuwashawishi viongozi hao ili kumaliza tofauti zao na kuliunda kundi mpya kwa nguvu kubwa. Katika mpango huu ulioitwa GREATER AGAIN umegawanyika katika phase na phase ya kwanza ni Kufanya MARIDHIANO kwa maasimu 2 katika siasa. Phase hii inaitwa kwa jina la RE-ESTABLISHMENT.

Ushawishi unaotumika ni kuwakutanisha na kusuluhisha tofauti yao kwa kuwapa mkakati wa kuhakikisha watoto wao wanachukua URAIS 2025. Maandaliz hayo yameshaanza kufanyika namna ya kumfanya mtoto wa R1 kuchukua form na mtoto wa R2 kuwa waziri Mkuu.

Mtoto wa R2 kwa mara ya kwanza atagombea ubunge jimbo la Monduli ili akidhi vigezo vya kuwa waziri Mkuu kwani katiba inatamka dhahiri kuwa ili uwe waziri Mkuu lazima uwe Mbunge wa KUCHAGULIWA.

Aidha imeandaliwa kuwa R1 au R2 itaamuliwa agombee upande upi Kulingana na hali itakavyokuwa.

Mpango huu umekuja baada ya kuona msimamo wa Mh. Rais Magufuli hauko upande wao hivyo wakaamua kujipanga ili Chama kisije leta Mtu mwenye mlengo wa kijamaa na itikadi za mwalimu na misimamo kama ya Rais Magufuli.

Kundi hili ndio hao waliokuwa wakipitisha mizigo bila kulipia kodi, ndio hao waliokuwa wakiruhusu mizigo itoke bandarini bila kulipiwa Kodi, Kuuwa tembo na kusafirisha twiga hai, Waingizaji na wauzaji wa madawa ya kulevya, waliojihusisha na Wizi wa MABILION YA SHILINGI katika Serikali YETU, ndio hao waliouwa shirika la ndege ATC na Shirika la Reli nchini nk.

Ikumbukwe maendeleo yoyote yanayoletwa na serikali hatuna budi kuyalinda. Hivyo kutokana na kuwepo kwa mpango huu nashauri yafuatayo

1) Viongozi wa Chama wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama wajiandae mapema kuwakabili ili kunusuru mpasuko wa kisiasa zaidi ya ule wa 2015.

2 ) Mipango ya namna hii isipewe nafasi hata kidogo kwa kuhakikisha tunaianika na kuikemea mapema

3 ) Viongozi wa chama wasiyumbishwe kwa ajili ya kutaka kuendelea baada ya awamu ya 5 na kukubali kununulika ili kufanikisha mipango ya namna hii.

4 ) Tusijisahau

5 ) Lazima wanachama tushikamane ili kupambana na nia Ovu za namna hii ndani ya CHAMA CHETU.

6) Kauli ya LOWASA kwamba marafik zake waliobaki CCM waendelee kushirikiana tusiiipuuze hata kidogo.

Tutaendelea kuhabarishana Kitakachokuwa kinajili katika mpango huu mchafu hasa kwa Phase inayoendelea.

VIVA MAGUFULI VIVA CHAMA CHA MAPINDUZI

NA
CHIKAWE JR.
Hii taarifa japo haiaminiki lakini si busara kuipuuza.
 
tozi25

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
5,956
2,000
Duh mkuu na mimi naitaka hio bangi uliovuta nije na uzi wa kijinga kama huu. Manake jana kuna mpemba aliniuzia bangi ya kipemba nikakiongea kipemba kumtongoza mwanamke wa kipemba.

Ndukiiiii
 
kabanga

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
37,045
2,000
Unazungumzia kwa ndabasi ya rafiki zako ambao umekuwa nao kipindi baba zenu wanakula pesa zetu
 
John-Q

JF-Expert Member
Oct 4, 2016
562
1,000
Hiyo greater again si ndio ile kauli mbiu ya Trump!

Ila isijekua muandishi ulichokiandika ndio conspiracy!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom