soma hii post kwenye red.Huyo c mwana chadema.
Napenda kuwashauri CHADEMA watekeleze mambo matatu yafuatayo ili kuondoa propaganda chafu zinazosambazwa na CCM na ambazo zinaweza kuwa na athari mbaya kwa chama chetu.
Wana-CHADEMA,tunapaswa kutambua kuwa watu tunatofautiana katika uelewa wa mambo na katika mapokeo ya taarifa tunazoletewa au kuzisoma.
Kwa maana hiyo basi,mambo haya nashauri yatazamwe upya.
1.Ukomo wa kugombe uongozi urudishwe katika katiba ya chama na ikiwezekano ukomo uwe ni vipindi vitatu vya miaka mitano mitano.
2.Wanachama waruhusiwe kwenda mahakamni na mtu akishindwa kesi aruhusiwe kuendelea na uanachama wake.
3.Mh.Mbowe,kipindi chako cha sasa kikiisha,nakushauri usigombee tena na utoe fursa kwa wengine kugombea na wewe kama kiongozi, ujikite katika kuhakikisha chama kinapata mrithi bora,wa kuamimika na mwenye viwango.
Mchango ndani wako ndani ya chama ni mkubwa na wa kuthaminiwa sana ila ni vizuri sasa ukatoa nafasi kwa wengine ili kukinusuru chama na propaganda hizi.
4.Japo hatuchagu kiongozi kwa kuangalia kabila lake, lakini ikiwezekana katika uchaguzi wa mwenyekiti ajae jambo hili likaangaliwa kwa mapana na marefu yake.
Wenye akili na upeo wa kuona mbali watanielewa, ila wenye kukariri kuwa chama hakihitaji ushauri wa aina hii, watakuja hapa na vijembe na kejeli.
Niwaambie tu,hata kiburi na kujiamini kwa Zitto msingi wake ni uwepo wa hizi propaganda na ndio maana hata anapata public sympathy kutoka kwa baadhi ya watu na watu hao ni wengi tu huku mitaani tunakoishi.Fanya utafiti mdogo uone.
Propaganda zingine ni za msimu tu lakini sio hizi nilizoziongelea hapa.
Yangu ni hayo tu.