Freeland
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 14,481
- 10,222
Msanii mkongwe wa Hip Hop na mbunge wa Mbeya mjini, Mh Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameachia wimbo wake mpya ‘Freedom’ ambapo ndani ya wimbo huo amezungumzia mambo mbalimbali yakiwemo mafanikio yake.
Mkurugenzi wa Hotel Desderia Co Ltd Mr Joseph Mbilinyi na Eng. Chao Nan wa kampuni ya ukandarasi Home Africa Investment Co Ltd ya China wakisaini mkataba wa ujenzi.
Mkurugenzi wa Hotel Desderia Co Ltd, Mr Joseph Mbilinyi na Eng. Chao Nan wa kampuni ya ukandarasi Home Africa Investment Co Ltd ya China wakisaini mkataba wa ujenzi.
Katika ‘Verse’ ya pili ya wimbo huo, Sugu amesema “Mama Hemedy mwanao nimefika mbali, maisha yana afadhali nakomaa ili nisifeli, kiukweli hata mwenyewe najikubali najenga mpaka hoteli!,” .
Pia hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa instagram alipost picha ya ujenzi wa hoteli hilo na kuandika: Mkurugenzi wa Hotel Desderia Co Ltd Mr Joseph Mbilinyi na Eng. Chao Nan wa kampuni ya ukandarasi Home Africa Investment Co Ltd ya China wakisaini mkataba wa ujenzi. Kampuni hiyo itajenga hotel ya nyota 3 itakayoitwa Hotel Desderia jijini Mbeya na ujenzi unaanza mara moja kwa mkopo wa bank ya CRDB.
Katika post nyingine ya hivi karibuni aliandika: Mkurugenzi wa Hotel Desderia Co. Ltd ya jijini Mbeya Joseph Mbilinyi akiwa kwenye makabidhiano ya site na wakandarasi wa Home Africa Investment Corp Ltd ya China… Mchakato wa ujenzi wa hotel hiyo ya nyota 3 umeanza rasmi leo… Mungu aendelee kubariki. Amen.
Kwa Hisani ya Blogu ya Wnananchi....Blogu ya Ze super Bilioneaaaa wa town