Confusion ya Marafiki, Please help!

barikiwa sana HorsePower kwa mawazo mazuri.
Nashukuru sana
hapo kwenye RED ndo hasa kwenye kiini cha hii mada...
Kwa nini watu wengi wanafikiri kama mna tabia zisizofanana na hasa kama mmoja wenu ana tabia ambayo haipendezi machoni kwa watu basi na mwingine ataiga hiyo? kwa nini wasiangalie the other way around?
 
Last edited by a moderator:
kuna wengine marafiki lakini wachoyo kwenye michongo ya hela!
Mh! huyo sasa si rafiki ni mnafiki, maana rafiki yako huwezi kumficha pa kula, na atakuwa na choyo moyoni mwake, si mzuri huyo kaa naye mbali.usimchekee kutoka moyoni nawe muonyeshe meno tu!!
 
Naungana na wewe FP, hata mie sielewi

Wakati nakua nilikuwa na rafiki ambaye mama yangu hakumpenda kabisa
Na hakuwa anataka niwe rafiki yake, lakini mie tulipatana kweli
Alikuwa anapenda mshedede sana
But haikuwa inanisumbua

Hata ukubwani, the same
Nina kila aina ya marafiki, wa mjini na wa kijijjini
Na hainisumbui
 
hapo sasa ni kazi yangu kama rafiki kuongea naye kwa mambo anayoyafanya.... siyo kumkimbia
 
Mh! huyo sasa si rafiki ni mnafiki, maana rafiki yako huwezi kumficha pa kula, na atakuwa na choyo moyoni mwake, si mzuri huyo kaa naye mbali.usimchekee kutoka moyoni nawe muonyeshe meno tu!!
ha haaaa, lol! utajiju mjini hapa
 

Nafikiri ni mtazamo tu wa kijamii juu ya hili suala. Sina uhakika kama kuna tafiti iliyoweza kufanyika na kutupa jibu la moja kwa moja. Ila pia watu huamini kuwa uwezekano wa kuiga mambo mabaya ndani ya jamii ni mkubwa zaidi kuliko kuiga mambo mema!
 
uzuri wa ukubwani ni kwamba unaamua kufanya unalolitaka, full stop...
yaani wewe ukijiona ni mkubwa na bado unafanya vitu ambavyo huvitaki ila kwa sababu ya watu basi inabidi ujiulize mara kumi kumi.
 
huu ndo ubinafsi, it is all about nitapata nini toka kwa hawa watu....
kwa nini usiamue wewe kuwa waridi kwa hao wenye tabia zisizofaa? i.e. wao wanukie toka kwako

Exactly! Unaweza kuwa rafiki wa huyo anayedhaniwa kuwa na tabia mbaya na wewe mwenye tabia njema ukawa sababu ya yeye kubadilika. Hayo mambo ya mtu mzima kuwa na tabia flani mbaya eti kwa vile tu umefuatana na mwenye tabia mbaya ndio ILE tunayoiita KUBEBEWA AKILI!
 
Nafikiri ni mtazamo tu wa kijamii juu ya hili suala. Sina uhakika kama kuna tafiti iliyoweza kufanyika na kutupa jibu la moja kwa moja. Ila pia watu huamini kuwa uwezekano wa kuiga mambo mabaya ndani ya jamii ni mkubwa zaidi kuliko kuiga mambo mema!
Huu mtazamo unaniudhi sana....
kuna watu wanaogopa kabisa kupeleka rafiki zao nyumbani au maeneo yao sababu wanawaza watu watawafikiriaje....
 
Umeona eeh!
na hapo itabidi ujiulize kama kweli umeshakua au la.
yaani sijioni kabisa kufanya kitu kisichofaa sababu tu rafiki yangu anakifanya. sasa nitakuwa na tofauti gani na watoto wanaoiga cartoon? Pale kwangu hadi lafudhi ni ya Ben10, lol!
 
Mada yako imenifanya nijiulize "urafiki ni nini?" au "rafiki ni nani hasa?". Inakuwaje watu wanakuwa marafiki? au kujiona wao ni marafiki? au hata watu wengine kuwaona/kuwachukulia wao ni marafiki? Kuna vitu/attributes gani vinafanana kutoka uhusiano mmoja wa kirafiki na mwingine? Je inawezekekana kwa mfano A akawa ni rafiki wa B, na B akawa ni rafiki wa C lakini A na C wasiweze kuwa marafiki (hata kama wapo eneo moja)? Je ni nini madhumuni/matarajio ya mtu kuwa na uhusiano wa kirafiki na mtu mwingine?

Kujaribu kuchangia hoja yako (na indirectly kujibu baadhi ya maswali ninayojuliza hapo juu), nadhani kwenye urafiki kuna mambo ya msingi (kwa wakati huo?) marafiki wanakuwa wanafanana/kubaliana lakini pia inawezekana kuna mambo kadhaa (yasio ya msingi sana) mkawa mnatofautiana. Kwa maoni yangu, kama hakuna mambo ya msingi mnayofanana/kubaliana (kwa wakati huo, au uwezekano wa kuwepo kwa mambo hayo baadae), urafiki hauwezi kuanza. Lakini ili urafiki uwepo (uwe sustainable), ni muhimu/lazima kwa kila upande au upande mmoja ku compromise baadhi ya vitu hivyo vinavyotofautiana. Na kuna nyakati kunaweza kuwa na urafiki juu ya mambo fulani tu (kwa mfano watu wanakuwa marafiki, lakini urafiki wao unaishia ofisini/kazini tu).

Sasa ni nani ana compromise inategemea sana na mizania ya nguvu, uwezo na hata madhumuni ya kila upande juu au dhidi ya mwingine. Sasa hapa ndio tunaweza kupata majibu ya inakuwaje mtu mzima anakuwa influenced na tabia ambayo anaona sio nzuri? Mimi naweza kusema wakati mwingine hiyo influence inatokea taratibu kiasi sio rahisi muhusika "kuiona" kwa urahisi. Na wakati mwingine, inakuwa ni sehemu ya compromise ili kufikia malengo fulani au hata kusustain urafiki kwa ajili ya malengo fulani.
 
hakuna tatizo as long as hakuna kulazimishana kuiga tabia ya mwingine. ukijitambua what you like and what you don't like dunia inaenda.
hivi kweli mtu anaweza kukulazimisha kuiga tabia zake ambazo huzipendi?
 
Huu mtazamo unaniudhi sana....
kuna watu wanaogopa kabisa kupeleka rafiki zao nyumbani au maeneo yao sababu wanawaza watu watawafikiriaje....

Kwa hali ya sasa ni vyema kuishi maisha yako mwenyewe bila kuangalia jamii inasema nini ili mradi tu maamuzi yako yasiwaumize wengine. Saa nyingine kuishi maisha ya kuangalia jamii inasema nini unaweza kujikuta unaishi kama mfungwa kwa kufuata matakwa ya jamii badala ya matakwa yako mwenyewe.

Mabadiliko huanzia kwako, ukiamua kubadilika na jamii nayo itabadilika taratibu! tukiendelea kuogopa, hali itaendelea kuwa ni hiyo hiyo mpaka kwenye vizazi vijavyo.
 
Nimeshusha pumzi kuubwa baada ya kusoma hiyo para ya mwisho..... kuna point kubwa sana hapo. Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…