Sasa mkuu, kama mwenye sifa hizo hawezi kuwekwa na yoyote basi mantiki yako haiko sahihi, kwa sababu ulisema kila chenye mpangilio kina muwekaji, sasa iweje Mungu mwenye mpangilio mgumu kabisa kuliko vyote akose muwekaji?
Ndo maana nilikwambia unaassume
Aisee .....
Tafakari yako ina tatizo,sijui una tatizo la kusahau pia au nini,maana kwa mtindo huu tutapata tabu sana kuelewana
Tulianzia kwenye binadamu na nikakuambia kuwa,binadamu ni kiumbe ambacho uwepo wake UNATEGEMEA mazingira kilichomo,pamoja na hilo kina mpangilio,kutoka kwenye hatua hiyo kuna mambo mawili
1;Kupangiliwa
2;Uwepo wake kutegemea mazingira,yaani uhai wa binadamu hauwezi kuendelea kuwepo bila kuwa na mazingira yanayosapoti huo uhai
Kwa udhaifu huo wa aina hizo mbili tu ni LAZIMA huyu binadamu awe kwanza amewekwa hapo na lazima awe ametengenezwa au kuumbwa
On the other hand tuna Mungu,Mungu uwepo wake hauna utegemezi wowote ule,according to my knowledge,[kama unapinga hili thibitisha hapa hapa] Sasa huyu unawezaje kusema kuwa "lazima nae atakuwa amewekwa"?
Sijui kama unanielewa ndugu
Unaona mkuu tunarudi pale pale, hapo kwenye bold bado inathibitisha kuwa hata hiyo intelligence ya Mungu nayo imetokana na intelligence nyingine zaidi.
Jibu la hili liko kwenye hayo maelezo hapo juu lakini nitakupa mfano mmoja ambao utakusaidia kuona tatizo lako kwenye hili
Mimi nasema kuwa haya mahindi gunia moja yatakuwa yameletwa na Thomas,lakini haya magunia mawili hayawezi kuletwa na Thomas,wewe unakuja na kuniambia kuwa,kama Thomas alileta lile gunia moja basi ni lazima na haya magunia mawili yatakuwa yameletwa na huyo huyo Thomas
Mimi nikakuambia kuwa,nimesema kuwa Thomas anaweza kuleta gunia moja kwasababu uwezo wa mwili wake unaruhusu kubeba gunia moja lakini lakini uwezo wake hauwezi kuruhusu kubeba magunia mawili
Sijui kama hiyo falsafa imekuingia ndugu,ukitaka uielewe iweke kwenye ishu ya Mungu na binadamu hapo juu
Hapana mkuu huo si uthibitisho, kwa sababu hiyo mantiki yako ya intelligence from intelligence bado haiwi applicable kwa Mungu, (kwamba kuna intelligence ambayo imemuumba Mungu)
Kama tungekuwa tunaijua intelligence iliyomtengeneza Mungu hapo ungekuwa sahihi
Ukisoma hapo juu nadhani utaelewa hili kwa urahisi sana
Kama tunaona katika mantiki yako, Mungu ambaye ni intelligent zaidi anaweza asiwe na muumbaji, kwa nini useme mimi ni lazima niwe na muumbaji ambaye ni intlligent zaidi yangu?
Sababu nimezisema hapo juu na natumai utakuwa umenielewa!