Cody Gakpo atua rasmi Liverpool

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
207
453
Kiungo mshambuliaji mpya Liverpool Cody Gapko aliyesajiliwa kutoka klabu ya PSV ya Uholanzi msimu huu amehusika katika magoli 21katika mechi 14 za ligi kuu ya Uholanzi alizocheza.

Amefunga jumla ya magoli 9 na kutoa pasi za magoli (assist) 12, Liverpool wamemsajili Gapko kwa dau la pauni milioni 30 kukiwa na kipengele cha ongezeko mpaka kufikia pauni milioni 50.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 kabla ya kusaini Liverpool alikuwa akiwindwa na klabu ya Manchester United.

Liverpool na Waholanzi damu damu, hawa ni baadhi ya Waholanzi ambao wamepita Liverpool Dirk Kuyt, Ryan Babel,Gini Wijnaldum wakati Virgil Van Dijk yeye bado yupo pale katika viunga vya Annfield.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom