Code ya Mungu

Code ya Mungu

Bess

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2016
Posts
555
Reaction score
661
Imekuwa kawaida kwa watu kuficha ujumbe kwenye codes ili tu ufikiwe na kundi lengwa.
Vivyo hivyo Mungu naye hutumia Codes kuwafikia watu wake.

Code yake ni Roho wake. Ukiwa naye unafahamu mambo yake, unajua analotaka ufanye, unasikia anachosema wakati wowote na mda wowote.

Ni vigumu sana kuacha dhambi, hasa kama huna nguvu ya Roho wa Mungu ndani yako ya kuiacha.

Roho wa Mungu huondoa kiu ya dhambi, hukupa mawasiliano ya moja kwa moja na mbingu zilizokuumba.

Sasa, ni wito uokoke, mkiri Yesu awe Bwana na mwokoz wa maisha yako, ili utakaswe na kuondolewa dhambi. Ukiwa safi hayo ni makazi ya Roho Mtakatifu wa Mungu, naye hakika ataishi ndani yako, atakaa na wewe...unakuwa mfano wa hekalu la Bwana na makazi ya ufalme wa Mungu.

Hii ndio code ambayo Mungu huwasiliana na watu wake walio duniani.
 
Kuokoka ni nini?
Ni kugeuka, kuacha dhambi na kukiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana. Atakutakasa kwa damu yake unaokoka na adhabu za shetani hapa duniani, na mwisho adhabu ya Mungu baada ya maisha haya.
 
Amen....Muumba wetu mwenye upendo anasubili utii wetu kwake na kumuamini yeye ili atusafishe mbali na dhambi zote,tuanze maisha mapya kwa uwepo wa Roho wake ndani yetu
 
Ni kugeuka, kuacha dhambi na kukiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana. Atakutakasa kwa damu yake unaokoka na adhabu za shetani hapa duniani, na mwisho adhabu ya Mungu baada ya maisha haya.
Unaweza kuacha dhambi ukiwa hapa duniani?
 
Unaweza kuacha dhambi ukiwa hapa duniani?
Kwa kweli huwez, tena narudia huwezi., sasa kwa kuona hivyo ndio tukapewa Roho wa Mungu atusaidie kuishinda dhambi,

Huyu Roho akiwa ndani yako unakuwa na tabia za kimbingu, zako zinakufa na maisha yako yanakuwa mapya.
 
Haiwezekani hata kidogo. Tumuombe Mungu atupe mwisho mwema, tutubie kila siku kwa tunayoyafanya bayana na sirini ama kwa kujua ama kutojua.
 
Haiwezekani hata kidogo. Tumuombe Mungu atupe mwisho mwema, tutubie kila siku kwa tunayoyafanya bayana na sirini ama kwa kujua ama kutojua.
Toba ni muhimu, sana sana. Sasa mtu anayezini kila siku, anasema uongo kila siku, anaiba kila siku: unataka awe anatubu kila siku?

Huyu mtu ni lazima atubu dhambi na kuomba nguvu ya Mungu kuishinda dhambi
 
Huna uwezo wa kuishinda dhambi
 
Back
Top Bottom