Kampeni ya ‘Chupa la Machupa’ imepelekwa rasmi Forodhani, Zanzibar, kuleta msisimko mpya katika mandhari ya eneo hili maarufu mjini Zanzibar.
Forodhani ni eneo lililopo katikati ya Mji Mkongwe, kati ya Jumba la Makumbusho na Ngome Kongwe, ni kivutio kikubwa cha wageni na wenyeji kila jioni, hasa kwa ladha zake adhimu za vyakula vya baharini. Kuanzia pweza, kaa, ngisi, kamba hadi barracuda – pamoja na urojo, sambusa, mihogo, kahawa ya viungo na pizza ya Zanzibar – eneo hili hujaza anga kwa harufu tamu na shamrashamra za watu kutoka pande zote.
Katika kutambua uzito wa utamaduni huu, Kampuni ya Coca-Cola imejumuika na jamii kwa kuleta ladha mpya kupitia kampeni ya ‘Chupa la Machupa’ inayosherehekea utamaduni, umoja na burudani. Kupitia chupa yake maarufu ya glasi ya 350ml, wateja wanapata fursa ya kushinda zawadi mbalimbali chini ya kizibo – kuanzia kinywaji cha bure kabisa, hadi punguzo la TSh 200 (asilimia 70) au TSh 500 (asilimia 30). Zaidi ya hapo, Coca-Cola huwafidia wauzaji moja kwa moja kuhakikisha mteja anapata kinywaji chake pasipo usumbufu.
Kwa wateja watakaokosa zawadi zao kwa sababu ya upungufu wa bidhaa eneo fulani, kampuni imeweka wazi namba ya msaada 0742 633 877 kwa ajili ya msaada na maelekezo ya mahali pa karibu pa kuchukua zawadi hizo.
Kampeni hii ya muda wa miezi miwili inalenga kuwafikia zaidi ya watu 100,000 kwa wiki, kwa lengo la kuwaleta karibu wateja waaminifu huku ikichangia kukuza biashara ndogo ndogo za Forodhani kwa kuongeza mauzo na kipato kwa wauzaji.
Lakini Coca-Cola imeenda mbali zaidi ya chakula pekee. Kampeni hii pia imesambaa hadi eneo la Makachu, maarufu kwa vijana wa Zanzibar wanaojirusha baharini katika mtindo wa kipekee, kuonyesha vipaji vyao na kuwakilisha utamaduni wa pwani. Katika muktadha huu, waogeleaji waliibeba Coca-Cola kwenye mabango, glasi na chupa, wakiruka kwa ustadi na msisimko mkubwa – tukio lililowakutanisha watu, kuwaleta karibu, na kuwa burudani ya kipekee inayobeba alama ya kampeni hii ya furaha.
Kwa mujibu wa wachambuzi wa burudani na utamaduni wa mitaani, kampeni ya ‘Chupa la Machupa’ ni mfano halisi wa jinsi chapa kubwa inavyoweza kuungana na jamii, kwa kuenzi utamaduni wao, kuongeza thamani ya maeneo ya urithi kama Forodhani, na kurudisha furaha katika kila kizibo.