CNN: Kuiwekea vikwazo Iran kunaidhoofisha USA

CNN: Kuiwekea vikwazo Iran kunaidhoofisha USA

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
CNN: Kuiwekea vikwazo Iran kutaidhoofisha Marekani
Kanali ya televisheni ya Marekani CNN imeripoti kuwa, kutounga mkono Ulaya hatua ya Marekani ya kuiwekea vikwazo Iran kutazidi kudhoofisha nguvu za Marekani.
Samantha Vinograd, mchambuzi wa kanali ya televisheni ya CNN ameashiria hatua ya serikali ya rais wa Marekani Donald Trump ya kuiwekea tena vikwazo Iran na kueleza kwamba, vikwazo hivyo vya nchi hiyo ni vya ubabe na utumiaji mabavu tu.
Sambamba na uchambuzi huo, kanali ya televisheni ya CNN imeonyesha taswira za maandamano ya jana ya wananchi wa Iran ya kuadhimisha Siku ya Taifa ya Kupambana na Uistikbari.
Siku ya Ijumaa iliyopita, serikali ya Marekani ilitangaza kuwa kuanzia leo Jumatatu itaanza kuiwekea tena Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vikwazo vinavyohusiana na masuala ya nyuklia.
Wakati huohuo mawaziri wa mambo ya nje na wa fedha wa Ujerumani, Uingereza na Ufaransa pamoja na Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya wametoa taarifa ya pamoja na kueleza kwamba, zimepigwa hatua kubwa katika kufanikisha utekelezaji wa utaratibu wa mabadilishano ya kifedha uliopendekezwa na EU, ambao unajulikana kama SPV. Lengo la kutumiwa utaratibu huo ni kuendelezwa uhusiano wa kibiashara na kibenki kati ya Umoja wa Ulaya na Iran katika kipindi cha vikwazo vya Marekani..
 
Hiyo Tv ya CNN kwa muda mrefu sasa imekuwa Pro Dems hivyo lazima watafute mtu wa kumhoji ambaye ana mwelekeo wa kuunga mkono sera za Democrats.

Hakuna namna ya kuwalazimisha Iran waache kuunga mkono vikundi vya kigaidi, njia pekee kwa sasa ni vikwazo tu make hamna namna.
 
Hiyo Tv ya CNN kwa muda mrefu sasa imekuwa Pro Dems hivyo lazima watafute mtu wa kumhoji ambaye ana mwelekeo wa kuunga mkono sera za Democrats.

Hakuna namna ya kuwalazimisha Iran waache kuunga mkono vikundi vya kigaidi, njia pekee kwa sasa ni vikwazo tu make hamna namna.
Vimefeli mkuu, kabaki Marekani peke yake, watu wananyonya wese tu Tehran....Tena wababe wenzie[emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom