Club Bingwa Africa: Simba SC inakwenda kuweka rekodi mpya kabisa!

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
10,052
24,442
Ni ngumu kwa baadhi ya mashabiki wenye mrengo fulani hivi kuamini, lakini huu ndio ukweli! Simba inakwenda kuweka rekodi mpya kabisa kwa kizazi hiki kwa kufika mbali sana kwenye mashindano ya Club bingwa Africa!

Ni wazi kabisa kwenye group lake hakuna wa kumzuia kuongoza ama kuingia robo fainali hadi hivi sasa!

Mechi ngumu ilikuwa ni kati yake na Al Ahly ambapo imekwisha na Simba ikajinyakulia point tatu muhimu na kuongoza kundi!

Na pengine mechi ya maridiano na Al Ahly kwao itakuwa ngumu, pia ila naamini vijana watakaza pengine kushinda ama hata sare!

Zimebaki mechi nne mzunguko wa makundi uishe, kwa kiwango cha Simba ilichonacho hivi sasa uwezekano wa kushinda mechi zaidi ya mbili kati ya hizo zilizobaki na kujikatia tiketi ya kucheza robo fainali ni mkubwa sana!

Zipo dalili za kila aina zinazoonyesha kuwa simba anaweza kuongoza katika kundi lake, na endapo itakuwa hivyo basi robo fainali atacheza na atayemaliza nafasi ya pili kutoka katika makundi yanayoshiriki, na hiyo itakuwa ni do or die hadi kieleweke, simba itaingia nusu fainali!

Na kitakachowashangaza wengi ni matokeo ya nusu fainali kuwa ya kuduwaza hasa wale wasioipenda Simba na mafanikio yake!

Mechi ya fainali itaacha historia ya karne kwenye kizazi hiki!

Viva Simba
 
Serikali ichunguze na kuifatilia kwa karibu timu ya Simba kwa ukibaraka wake kwa Mabeberu. Aiwezekani timu ya Simba kucheza soka la Ulaya wakati apa Tanzania tuna sokaletu la kizalendo la kusukumana,kupandishiana miguu kichwani,kulima kwa miguu uwanjani,kupigana ngumi kama Niyonzima n,k.

Simba wanapiga pasi kama Eniesta,Xavi,Zizu na kufunga magoli ya ki-Messi Messi wakati ao ni wachezaji wa Ulaya kwa Mabeberu.

"Alisikika mlevi mbwa mmoja akiwa mitaa ya Jangwani akilalamika kwa uchungu mkubwa"
 
Tuna benchi la ufundi lililo kamilika ipasavyo,tuna team nzuri sana iliyobalance,uongozi safi kabisa ,maandalizi mazuri sioni sababu kwanini isiwezekane.....all the best mnyama
giphy.gif
 
Utopolo ni lazima mtoe povu! Eti record gani...
Tayari unaleta siasa. Mie sio utopolo mkuu naongea ukweli, mpira hasa virabu vya tanzania ni homa za vipindi na siasa. Ikatokea hapo simba akapigwa mechi mbili tatu, tayari mnageuka na kuanza tukana, sasa hizo ni akili au uchafu kwenye kichwa
 
Siasa gani nimeleta sasa?
Wewe ni utopolo kwa sababu ulicomment kiutopolo! Ulivyouliza record gani, huo si utopolo? Kuwa club ya kwanza kwenye makundi kufikisha point 6 bila kufungwa si record hiyo...!?

Hao wanaotukana akili zao hazina tofauti na zako!
 
Unaona mafanikio hayo ? Basi kama hayo kwako ni mafanikuo na ni record basi bado mpira wa bongo una safari ndefu sana
 
Unaona mafanikio hayo ? Basi kama hayo kwako ni mafanikuo na ni record basi bado mpira wa bongo una safari ndefu sana

Wewe kwako mafanikio ni nini?
Kuna mafanikio yasiyo na hatua...!? Huwa mafanikio yanaibuka tu from nowhere kwa hiyo...?

Kama hayo unaona si mafanikio basi unapaswa kuitwa utopolo square!
 
Mimi naita huu ni ushamba wa kisoka,kwa klabu kama simba haikupaswa kuona haya matokeo kama miujiza na kuja kujaza server za Jf. Na kwa hii mihemko mliyonayo hamuendi kokote,kwa sababu kwanza hamjiamini. Ulikuwa ni wajibu wenu kupata matokeo mazuri,acheni kusumbua watu
 
Pole sana kwa kuteseka uto subiri tufike final ndiyo mtajua hamjui punguwani waheed wewe.
 
Wewe kwako mafanikio ni nini?
Kuna mafanikio yasiyo na hatua...!? Huwa mafanikio yanaibuka tu from nowhere kwa hiyo...?

Kama hayo unaona si mafanikio basi unapaswa kuitwa utopolo square!
Subiri mtapo pelekewa moto.. ndio tutapa ukweli wa rangi zenu
 
Back
Top Bottom