Clouds yatoa ufafanuzi malipo ya TSh milioni 629 yaliyotajwa na CAG

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,390
5,310
Meneja wa fedha wa kampuni ya Clouds Media Group, Issa Masoud amesema walitoa vielelezo vyote ikiwa ni pamoja na stakabadhi kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kufuatia malipo ya Sh 629.7 milioni kwa ajili ya matangazo ya tamasha la urithi mwaka 2018.

Masoud ametoa ufafanuzi huo leo Alhamisi Aprili 8, 2021 katika kipindi cha Traffik Jamz kinachorushwa na redio Clouds saa chache baada ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kueleza kuwa Clouds ililipwa kiasi hicho cha fedha lakini hakukuwa na risiti zozote za kielektroniki zilizotolewa kuthibitisha malipo husika.

Katika ripoti hiyo ya CAG, imeeleza kuwa televisheni ya Clouds walilipwa Sh 629.7milioni na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Sh201.4 milioni kwa ajili ya kuonyesha matangazo ya tamasha hilo.

Akizungumza leo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma CAG, Charles Kichere amesema kodi ya zuio ya Sh31 milioni na Sh10 milioni kutoka Clouds na TBC hazikukatwa kutoka katika malipo hayo.

"Wizara haikutimiza wajibu wake katika kukata hiyo kodi ya zuio, vilevile sikupewa ushahidi ukionyesha kuwa manunuzi ya huduma za matangazo kutoka TBC na Clouds yalipatikana kwa ushindani ulio sawa.”

“Pia nilibaini Sh487 milioni zilipelekwa kwenye taasisi saba kwa ajili ya utekelezaji wa tamasha hata hivyo hakukuwa na nyaraka zilizowasilishwa kwa wakaguzi kuthibitisha matumizi hayo,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Ifahamike kuwa ripot ya CAG inakuwa ni uhalisia wa kila jambo. Wakaguzi hawaondoki sehemu pasipo kupata maridhiano ya pande zote mbili kukubali.

Mfano mimi nimenunua kitu cha laki 3 na sina risiti. Mkaguzi akija kuuliza risit ipo wapi, nikamwambia sina au nikatoa ambayo ni nje ya utaratibu. Basi mkaguzi yeye ataandika ule uhalisia.

Ndo maana huwezi ukakuta mabenki, taasisi, vyama n.k vinapinga uhalisia wa ripoti ya mkaguzi.

Ifamike pia, kabla CAG hajasoma hizo hesabu zake, mashirika kama ATCL, TPA wanajua kabisa ni madudu gani katika mashirika yatakwenda kuwekwa wazi. Wanajua kabisa kuanzia sehemu ya kwanza mpaka ya mwisho.

Ni aibu kubwa kwa taifa kumjibu CAG kienyeji enyeji tu.
 
Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa??

*Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.
*
Muda utaongea .
 
Meneja wa fedha wa kampuni ya Clouds Media Group, Issa Masoud amesema walitoa vielelezo vyote ikiwa ni pamoja na stakabadhi kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kufuatia malipo ya Sh 629.7 milioni kwa ajili ya matangazo ya tamasha la urithi mwaka 2018.

Masoud ametoa ufafanuzi huo leo Alhamisi Aprili 8, 2021 katika kipindi cha Traffik Jamz kinachorushwa na redio Clouds saa chache baada ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kueleza kuwa Clouds ililipwa kiasi hicho cha fedha lakini hakukuwa na risiti zozote za kielektroniki zilizotolewa kuthibitisha malipo husika.

Katika ripoti hiyo ya CAG, imeeleza kuwa televisheni ya Clouds walilipwa Sh 629.7milioni na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Sh201.4 milioni kwa ajili ya kuonyesha matangazo ya tamasha hilo.

Akizungumza leo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma CAG, Charles Kichere amesema kodi ya zuio ya Sh31 milioni na Sh10 milioni kutoka Clouds na TBC hazikukatwa kutoka katika malipo hayo.

"Wizara haikutimiza wajibu wake katika kukata hiyo kodi ya zuio, vilevile sikupewa ushahidi ukionyesha kuwa manunuzi ya huduma za matangazo kutoka TBC na Clouds yalipatikana kwa ushindani ulio sawa.”

“Pia nilibaini Sh487 milioni zilipelekwa kwenye taasisi saba kwa ajili ya utekelezaji wa tamasha hata hivyo hakukuwa na nyaraka zilizowasilishwa kwa wakaguzi kuthibitisha matumizi hayo,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
Kipanya siyo wa kumwamini hata chembe!
 
Back
Top Bottom