Clouds TV mnatia aibu

Mulangila Mukuru

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
1,945
728
Jana Clouds TV wakitangaza taarifa ya habari ya saa 2:00 usiku waliandika jina la rais wa JMT walimwandika kama JOHN PIMBE MAGUFULI hili ni kosa dogo la kiuandishi lakini wahariri hii ni aibu kwenu kulikosea jina la Rais kuanzia mwanzo wa taarifa mpaka mwisho jirekebisheni.

5a6ac0d149db125874013d8ec5126cb5.jpg
 
Jana Clouds TV wakitangaza taarifa ya habari ya saa 2:00 usiku waliandika jina la rais wa JMT walimwandika kama JOHN PIMBE MAGUFULI hili ni kosa dogo la kiuandishi lakini wahariri hii ni aibu kwenu kulikosea jina la Rais kuanzia mwanzo wa taarifa mpaka mwisho jirekebisheni.

5a6ac0d149db125874013d8ec5126cb5.jpg
Huko sijui ni kukosa kazi au ni ujuha tu hata sielewi.. Kwahyo hyo ndio sababu iliyokufanya uwahi asubuhi yote hii kuja kuandika hapa,?
 
Wahariri si ndo akina Adam Mchovu kuna Mhariri aliyesoma Clouds?

Mhariri wao ni Jerome Risasi mwenye Advance Certificate ya DSJ ya miaka 10 au 12 iliyopita huku akiwa na uzoefu mzuri tu kama News Reporter na Photoghrapher wa Vyombo vya Habari mbalimbali. Ninachojiuliza tu ni sijui ni kwanini aliyekuwa Mhariri Mkuu na Bosi wa Jerome Risasi Mwanadada Joyce Shebe ambaye anamzidi kwa mbali sana Kielimu na Kiuzoefu amekuwa demoted na Management ya Clouds Media Group na nafasi yake kupewa Jerome Risasi Mtoto wa Kawe Kindakindaki.
 
Ni kawaida sana kutokea
Tusitetee ujinga kwa kivuli cha kawaida sana kutokea! Mhariri una kazi gani? Boss wangu alikuwa na kawaida ya kutuambia kabla hujatuma ripoti kwenye mtandao hakikisha umeisoma, umeisoma na umeisoma! Maanake nini? Kama kuna typing errors utakuwa umeziona na kurekebisha, sasa mihariri hopeless kama Shindu Namwaka inapokea na kurusha hivyo hivyo utafikri inawahi nyumbani kukamata ugoni!
 
Hiyo typo error mimi huwa naona katika tv zote za ndani huku ZBC ikiwa kinara pamoja na umahiri wao wa kuongea lugha kwa ufasaha
ZBC sio hawana weledi wa kiswahili. Wanaijua vizuri ile lugha ya mashariki ya kati
 
Clouds ichukueni hiyo taarifa ya mleta uzi kama changamoto kwenu katika zama hizi za ushindani,sio nyie tu mnaokosea lakini neno zuri la kiungwana ni kuwaomba radhi wasikilizaji/watazamaji wenu kwa usumbufu walioupata.
 
Back
Top Bottom