Ifike mahala nchi yetu itambue mihimili minne ya dola yenye kujitengemea pasina kuingiliana kiutendaji na kimaamuzi. Mihimili hiyo iwe:
1. Bunge
2. Serikali
3. Mahakama
4. Media
Tatizo lililopo kwa sasa ni kwamba huo mhimili namba 4 hapo juu umefichwa lakini unaonekana kutumiwa sana na mhimili namba 2 ktk kupotosha wananchi na kuendelea kujihalalishia utawala wake.
Suala la chombo cha habari kusambaza ujumbe potofu unanipa shaka kuamini umakini na weledi wa mhariri ama msimamizi wa matangazo ktk media husika.
Tufike mahala tuamue kuwa wakweli pasipo kutegemea hongo kutoka kwa watawala na hii itawezekana tu endapo wamiliki wa media watatimiza jukumu na wajibu wao wa kulipa kodi halali serikalini hivyo kuondoa mazingira ya kuamuliwa cha kuhabarisha na kuripoti kwa wananchi kwa usahihi wake.