Clouds mtawatumia wasanii mpaka lini?

Decree Holder

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
2,556
3,741
HISTORIA YA MIRABAHA TANZANIA

Tanzania ilikuwa na sheria ya Hakimili kuanzia miaka ya 1920, hii ilitokana na kuwa nchi hii ilikuwa koloni la Uingereza na hivyo kufwata sheria za Uingereza katika haki hizo.

Mwaka 1966 Tanzania ikapata sheria mpya ya hakimiliki iliyoitwa Copyright Act no 61 ya 1966. Ambao ilikuja kuboreshwa na Sheria ya hakimiliki na Hakishiriki na 7 ya 1999. Kabla ya mwaka 1964 redio iliyokuwepo TBC ilikuwa ikilipa mirabaha kwa matumizi ya muziki katika vipindi vyake. Watangazaji walijaza log sheets zilizoeleza nyimbo walizotumia na pia kujaza needle time, au muda wa urefu wa wimbo, ili kutayarisha hadidu rejea za malipo kwa nyimbo zilizopigwa.

Katika miaka hiyo radio hiyo iliacha kulipa mirabaha na kwa miaka yote mpaka leo kiasi cha miaka 50 kumekuweko na utamaduni wa matumizi ya muziki na vyombo vya utangazaji bila kulipia mirabaha. Hakika kuondoa utamaduni wa kutumia kazi bure si jambo rahisi. Mwaka 2003, kanuni za ulipaji mirabaha zilipitishwa, lakini toka wakati huo vyombo vya utangazaji havijawahi kulipa mirabaha. Moja ya sababu kubwa ni kuwa, vyombo hivyo viliona kuwa vikilipa fedha hizo hazitawafikia wanamuziki husika.

Hatimaye mwaka 2015, teknolojia ya kuweza kujua redio na TV gani imepiga nyimbo gani na kwa wakati gani, imeingia nchini hivyo swala la kujua mirabaha alipwe nani na kwa bei gani si tatizo tena.
Pamoja na ufumbuzi huu, kumeanza kutengenezwa mazingira ya kuendelea kutokulipa mirabaha kwa kuanza kutoa visingizio mbalimbali na hata kutumia kundi dogo la wanamuziki ambao hawajaelewa sawasawa utendaji wa sheria hii kupinga kulipwa.

Jambo ambalo hakika litachekesha ulimwengu wote kwani itakuwa ni mara ya kwanza wanamuziki wa nchi ya Kiafrika kukataa kulipwa mirabaha na kung’ang’ania kazi zao ziendelee kutumika bure.

Hakika watu wengine hawatapendelea taratibu za ulipaji wa mirabaha, kwani utaratibu huu utalazimisha radio kutafuta nyimbo bora za kupiga na hivyo kuwaondolea kitumbua wale waliokuwa wakitumia rushwa kuhakikisha nyimbo zao zinapigwa hata kama si nzuri.

Utaratibu huu utaweka wazi mapato ya redio TV na hivyo kuwezesha ukusanyaji kodi bora kutoka vyombo vya utangazaji, utaratibu huu utawezesha wadau wengine katika muziki kama vile producers, watunzi wa muziki na maneno, publishers nao kuanza kufaidi mapato ya kazi zao, utaratibu huu, utawezesha wanamuziki ambao hawako tena majukwaani lakini kazi zao bado zinapigwa hewani kupata kipato kutokana na kazi hizo.

Kukusanywa kwa mirabaha ya kazi za nje kutawezesha fedha nyingi za wanamuziki zinazokusanywa kwa nyimbo zilizopigwa na vyombo vya utangazaji vya nje kuweza sasa kulipwa kwa wanamuziki hao.
PIGENI MUZIKI KWA HAKI, LIPENI MIRABAHA KWA HAKI


Kakundi hako kadogo kapo chini ya clouds juzi wamekutana na kuahirisha malipo ya mirahaba pasi na sababu za msingi.
 
Swali lilipaswa liwe wasanii wa Tanzania watatumiwa na Clouds mpaka lini ?
 
Back
Top Bottom