Clouds Media International yafungua ofisi Jamaica

Clouds Media International yafungua ofisi Jamaica

Nukta5

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2014
Posts
1,192
Reaction score
1,315
Ufunguzi wa ofisi mpya nchini Jamaica unakuja ikiwa hata mwaka mmoja haujapita toka Clouds Media International ilipofungua ofisi zake Abu Dhabi.

Mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media, Joseph Kusaga amesema ufunguzi huu ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu kuiwezesha kampuni yake kujitanua kimataifa ikiwa ni pamoja na uzalishaji na usambazaji vipindi, utoaji wa huduma za ziada kupitia simu za mkononi, masoko na usimamizi wa matamasha bila kusahau matumizi ya solar na vyombo vya habari.

"Jamaica na Caribia kwa ujumla ni soko jipya kwetu na kama Clouds mara zote huwa tunafikiria ni kwa namna gani tunaweza kujipenyeza katika masoko mapya ili kujitanua na kufanya biashara endelevu hivyo tunaona hii ni sehemu ya muafaka wa bidhaa na huduma tunazotoa" – Joseph Kusaga.

Shughuli zote za Clouds International zitasimamiwa na Dean Mundy, mtayarishaji wa muziki wa reggae na mfanyabiashara mzawa wa Jamaica mwenye uzoefu katika ukanda huo ambapo kukamilika kwa uzinduzi wa ofisi hizi kunadhihirisha umakini wa Clouds kujitanua kimataifa.

"Ni zaidi ya muongo mmoja sasa toka nilipokutana na Joe na wenzake nilipokuja Dar es salaam kwenye tamasha la Fiesta na haikunichukua muda kutambua kuwa hii ni kampuni ambayo tunaweza kufanya nayo kitu, japo kwa hakika sikujua ni kivipi ila kwa sasa uhakika ninao na pia fursa zipo, tuko tayari kufanya vitu vikubwa hapa Jamaica" – Mundy

Pamoja na Clouds Media International, makampuni tanzu kama status communications, Primetime International na Ray's Solar yatakua na makao yake Kingston, ambapo status communications itajihusisha na utoaji huduma za ziada kupitia simu za mkononi, Primetime International itasimamia uandaaji wa matamasha na usimamizi wa Wasanii huku Ray's Solar ikitoa huduma za umeme wa mionzi ya jua.

http://www.bongo5.com/clouds-media-international-yafungua-ofisi-jamaica-08-2014/
 
Kusaga ndo anaye imiliki hiyo Clouds International yenye makao yake makuu Abu Dhabi??
 
-Kama ni kutanua soko kimataifa, kwanini wasianze na Bara la Africa hususani nchi jirani?
-Kwanini hawajatupatia japo vipicha vya hizo ofisi za abu dhabi na kule nyumbani kwa kina usain bolt tuzione?

Nadhani Huu Ni Muendelezo Wa Zile Movie Zao.
 
clouds itakuwa kampuni kubwa endapo tu itaondoa watu wenye tabia mbovu ambao huamini kujidhalilisha nikukuza majina yao badala ya kuchapa kazi. Mungu awaongoze,mtafika tu.
 
Fursa za kutanua soko la mihadarati bado hapa tanzania tu soko halijawafikia wote wamekimbilia uae ghafla wameenda kwa wavuta bangi mmmmhhhhhh...Mchomvu aende kuwa mtangazaji wa clouds jamaica.
 
Quote: "Niggaz ain't getting money, but they have an opinion." Big up to clouds Group.
 
Back
Top Bottom