nguvumali
JF-Expert Member
- Sep 3, 2009
- 4,927
- 1,342
Clouds media tayari wamezindua msimu wa Burudani za Fiesta kule Mkoani Kigoma, itafuatiwa na matamasha kadhaa katika mikoa zaidi ya kumi (10) .
Wapenda Burudani katika mikoa hiyo wanajiandaa kupata burudani ya uhakika isiyo na mikwaruzo.
Leo tangu asubuhi kwenye radio yao inayosikika baadhi ya mikoa michache nimewasikia wakisifu tamasha la Kigoma kuwa lilifana na kinyume na matarajio yao.
tangu wameanza kuandaa maonesho yao hatujasikia popote waadaaji wengine wakijaribu kuingilia matamasha hayo especially katika mikoa ambayo burudani hiyo itarindima katika tarehe husika.
Wao clouds kupitia Prime time Promotion wamekuwa vinara wakuvuruga matamasha yawenzao hapa na pale. mfano mzuri tamasha la Vinega pale Ustawi wa JAMII miaka miwili nyuma na karibuni zaidi Tamasha la Judith WAMBURA pale Nyumbani Lounge....japo pamoja na majaribio yao matamasha yote ya Vinega na Jide yaling'ara.
WITO WANGU NI HUO , BURUDANI SI VITA JAPO NI BIASHARA ,......WAJIFUNZE USTAARABU SOKO NI KUBWA HAKUNA HAJA YAKUTOANA MACHO.